April 4, 2018




Na Saleh Ally
SISI Watanzania ni watu waungwana sana, hii imekuwa ni sifa tuliyoibeba kwa muda mwingi na yenyewe inatubeba pia, vizuri kusema tunabebana!

Lakini miongoni mwetu kuna wengi ambao wamekuwa na roho za wivu, husuda, wasiopenda maendeleo ya wenzao na mara nyingi wanahisi wanaonyeshewa au watu fulani wanajidai sana.


Wako wanaochukizwa na maendeleo ya wenzao bila ya kujikagua kwamba kweli wanajituma, wanafanya kazi bila kuchoka kirahisi na wanafurahia maendeleo ya wenzao?

Kufurahia maendeleo ya mwenzako, huo ni wivu wa kimaendeleo kwa kuwa lazima utatamani na wewe kufanikiwa. Usipofurahia maana yake ni kupinga na wewe hutafanya lolote.

Nilizungumzia hivi karibuni namna baadhi ya watu walivyojitokeza kumshambulia Abdi Banda mitandaoni, tena kwa matusi eti kisa alisema anashangazwa na kumuona Msemaji wa Simba, Haji Manara akilalama mbele ya vyombo vya habari sababu Simba haikupewa penalti dhidi ya Yanga.

Nilifafanua kuhusiana na uhuru wa kujieleza, Banda hakutukana, alitumia uhuru wake wa kujieleza na kile alichojifunza Afrika Kusini. Lazima tukubali sote hatuchezi huko, yeye anajua mengi ya huko na kitu kibaya zaidi wako ambao hamjafika ndiyo maana mnaweza kudharau kwa kuwa hamjui kilichopo.

Alichonifurahisha Banda, pamoja na matusi yote, hakuwahi kujibu, amekaa kimya na ameendelea kufanya kazi yake kwa ufanisi wa juu kabisa.

Hii inatosha kuwa jibu la kisayansi kwenu ambao silaha yenu ni matusi. Kawaida anayetukana ni asiye na uwezo wa kuchanganua hoja, ukimjibu mnaweza kufanana, Banda kaonyesha amepiga hatua na kweli kuna jambo amejifunza Afrika Kusini.

Kwa sasa nidhamu ya Banda iko juu, Banda anayecheza Baroka FC ya Afrika Kusini na yule wa Simba ni watu wawili tofauti. Wale mliomtukana, wale mlioona kilichokuwa kinaendeleza jifunzeni na ikiwezekana muamini kuwapa sapoti wachezaji wa Kitanzania pia ni kuisaidia Tanzania badala ya kukubali kutumwa kwa niaba ya watu.

Ukibahatika kufika Afrika Kusini utajifunza, hata timu ya Baroka FC niliyoishi nayo sehemu moja kwa siku mbili, ilitosha kwangu kujifunza. Wachezaji wana nidhamu ya juu, wanafika kwenye chakula kwa wakati mwafaka na wanaondoka katika eneo husika wakati sahihi.

Banda alitaka kubaki kuzungumza na mimi baada ya kula, alilazimika kumuomba meneja wake. Meneja wa timu akamuambia asubiri, akaomba ruhusa kwa kocha ndiyo ikapitishwa.




Wakati timu ilipoondoka, Banda alibaki hotelini kwa siku moja. Nikataka kumfanyia mahojiano nje ya tulipokuwa, kocha ndiye aliyetoa ruhusa kwa kuwa alijua ingeonekana amefanya mahojiano nje ya pale hata kama aliruhusiwa, ingekuwa kesi na adhabu juu ya faini ya Sh 900,000  ya Tanzania, kwa kila kosa moja. Tujifunze na tuonyeshe upendo, chuki hazina msaada kwetu.

7 COMMENTS:

  1. Naona mwandishi yupo obsessed na suala zima la Banda. Anajaribu kulazimisha tukubaliane naye. Banda tuliyemzoea ni yupi?Ameacha lini ujinga?Kumuona South Africa siku mbili ndio ushahidi tosha?Umemuuliza swali kashindwa kujibu na kuanza kulaumu ambalo hayaulizwa. Mfumo tulionao wasemaji wa klabu wanaisemea timu yao. Hajaona au kusikia Ugiriki Raid wa timu kaingia uwanjani na bastola kupinga maamuzi ya refa.Au
    Ulaya hakuona ajabu .Salehe ina haki ya kuamini unavyotaka lakini huwezi kulazimisha tufikiri unavyofikiri wewe.

    ReplyDelete
  2. Mwandishi, be professional please! Acha ushabiki

    ReplyDelete
  3. SALEH USITULAZIMISHE KUAMINI UJINGA ALIOONGEA BANDA SISI SIO WAJINGA WENZAKE TIMU YENYEWE TUMEIJUA BAADA YA YEYE KWENDA NA KULETA MIPASHO YAKE.

    ReplyDelete
  4. Atakuwa professional kwa lipi?Hajui hata ethics za journalism bali kuandika kwa mazoea. Kila anayeandika kwenye gazeti au blogg anajiita journalist bila kuwa na taaluma ya uandishi wa habari.

    ReplyDelete
  5. ndio mchezaji wa kwanza kwenda nje acheni uswahili wa magazeti na uchonganishi

    ReplyDelete
  6. hivi wewe ni mwandishi wa simba na yanga tu mbona hutoi live ya michezo mingine

    ReplyDelete
  7. Thomas Kohl hata kumuita mwandishi umempa ujiko labda mwandishi wa umma. Ukanjanja tu .

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic