April 3, 2018



Full Time Na mpiraa umekwisha, Simba wanaibuka kidedea kwa kujikusnayia alama 3 muhimu dhidi ya Njombe Mji FC
Dak ya 93, Simba wanatoa mpira nje, Njombe wanahi haraka kurusha 
Dak ya 92, Nyoni ameshapoga faulo
Dak ya 92, Ni faulo inapigwa kuelekea Njombe Mji, Simba wanajivuuta kwenda kupiga

DAKIKA 90 ZIMEMALIZIKA, ZIMEONGEZWA NNE


Dak ya 89, Goli Kiki, mpira unapigwa kuelekea Simba, wakati huo benchi la ufundi la Simba limeinuka kumlalamikia Mwamuzi baada ya kupeta faulo aliyochezewa Niyonzima
Dak ya 88, Matokeo bado ni 0-2, mechi inaendelea na dakika zinaelekea mwisho
Dak ya 86, Mbonde ameumia, yupo chini akigangwa, yawezekana akawa ameumia vibaya
Dak ya 84, Mpira umesimama tena, Kwasi yuko chini, tayari ushaanza
Dak ya 83, Njombe wanarusha kuelekea lango la Simba, karibu na eneo la goli, rushwa huku mpira unamkuta Mustafa, anapiga shuti kali, mpira unakwenda nje
Dak ya 81, Kichuya anatoka kumpisha Haruna Niyonzima
Dak ya 81, Nyoni sasa na mpira, mpira umesimama
Dak ya 79, Gyan anarusha mpira baada ya Njombe kuutoa, wakati huo Simba wakifanya mabadiliko, Niyonzima anaingia 

Dak ya 78, Beki wa Njombe anaparamiana na Mavugo akiuwahi mpira, piga mbele kuelekea langoni mwa Simba
Dak ya 77, Simba wamekosa bao la tatu, pichi ya Uwanja imeshindwa kustahimili mwendo wa mpira
Dak ya 74, Njombe Mji wanashindwa kufanya utulivu, nafasi nzuri wameshindwa kuitumia kupata bao
Dak ya 75, Nyoni anapewa kadi ya njano baada ya kuanza kubishana na Mwamuzi
Dak ya 72, Faulo imetoka eneo la hatari mwa Simba, inapigwa kuelekezwa Njombe Mji
Dak ya 71, Kapombe anapiga shuti moja la kushoto na mpira unakwenda nje ya lango
Dak ya 70, Njombe wanapata kona, wakati wakifanya mabadiliko, pigwa kona huku lakini ngome ya Simba inakuwa imara
Dak ya 69, Mbonde anatoa nje mpira katika harakati za kuokoa, unarushwa kuelekea Simba

Dak ya 68, Juuko anapata kadi ya njano baada ya kumkwatua mchezaji wa Njombe Mji
Dak ya 66, Hatari nyingine kwenye lango la Njombe, kipa anadaka
Dak ya 64, Boccooooo, anaifungia Simba bao la pili kufuatia kazi nzuri ya Shomari Kapombe
Dak ya 63,Njombe wanafanya shambulizi lingine la nguvu lakini linashindwa kuzaa matunda
Dak ya 60, Simba wanafanya mabadiliko, ametoka Kotei aliyeumia na nafasi yake imechukuliwa na Salim Mbonde

Dak ya 59, Mpira umesimama tena, Kotei ameumia
Dak ya 59, Hatari katika lango la Simba, Njombe wanakosa tena nafasi nyingine ya kupata bao
Dak ya 57, James Kotei anapewa kadi ya njano baada ya kucheza madhambi, mpira umesimama
Dak ya 55, Kocha Masoud Djuma amesimama kuhamasisha wachezaji wake wazidi kupambana
Dak ya 54, Kisu anaanza upya, piga mbele kuwatafuta washambuliaji wake, kwake Kasewa huku, faulo, inapigwa kuelekezwa Simba
Dak ya 52, Simba wanafanya mabadiliko, ametoka Okwi na nafasi yake imechukuliwa na Laudit Mavugo
Dak ya 49, Kona kuelekezwa Simba sasa, anapiga Bakari Mustafa, piga huku inaokolewa
Dak ya 48, Faulo inapigwa kuelekea Simba, nje kidogo ya eneo la 18, pigwa shuti kalii huku linakwenda sentimita chache nje ya goli
Dak ya 47, Simba wanapata kona ya kwanza, anapiga Kichuya, pigwa huku fupifupi, inaokolewa
Dak ya 45, Simba wameanzisha mpira

KIPINDI CHA PILI KINAANZA

Dak 45 za kwanza zimemalizika, sasa ni mapumziko
Dak ya 47, Mpira anao Nchimbi sasa, faulo tena, inaelekezwa Njombe mji
Dak ya 46, Mpira unarushwa kuelekea Simba

DAKIKA 45 ZIMEMALIZIKA, ZIMEONGEZWA TATU

Dak ya 44, Pigwa mbele huku mpaka kwa kipa Manula, anadaka
Dak ya 43, Faulo kwenda Simba, Njombe wanapambana kusawazisha bao

Dak ya 42, Nchiiimbi, hatari, namna gani pale mpira umempita mguuni na kukosa kuipatia Njombe bao la kusawazisha
Dak ya 41, Simba wako katikati mwa Uwanja, Kichuya anampasia Okwi, kwake Bocco lakini Mlinzi wa Njombe anamuwahi
Dak ya 39, Mpira umesimama kwa muda, Manula anapewa huduma ya kwanza
Dak ya 38, Njombe wameamka zaidi wakitafuta bao la kusawazisha, wakati huo huo Manula ameumia
Dak ya 37, Njombe wanacheza faulo, piga mbele kabisa kule, Kwasi anaokoa

Dak 37, Mpira umetoka, unarushwa kuelekea Simba
Dak ya 36, Goli Kiki, mpira unapigwa kuelekea Simba
Dak ya 35, Faulo kuelekezwa Simba, Mustafa anapiga. Piga mbele huku inatokea ngonga nikugonge lakini Simba wanaokoa
Dak ya 34, Mchezaji  mmoja wa Njombe yupo chini, mpira umesimama
Dak ya 33, Njombe wanajitahada kupenya ngome ya Simba wanapopata nafasi lakini inakuwa vigumu kutokana na uimara wa beki ya Simba

Dak ya 31,  Njombe na mpira sasa, Kwasi anauchukua. Mwamuzi anapuliza filimbi, ni faulo kuelekea Njombe, Kwasi amechezewa madhambi
Dak ya 30, Faulo inapigwa kuelekezwa Njombe, Kapombe amefanyiwa madhambi, Juuko anapiga
Dak ya 28, Bocco sasa anaenda na mpira, anaparamiana na kipa wa Njombe, Mwamuzi anasema mpira uendelee, goli kiki
Dak ya 28, Tayari faulo ishapigwa na inaokolewa na mabeki wa Njombe, pigwa kuelekea langoni mwa Simba, na Manula anaanzisha upy

Dak ya 27, Mpira anao Manula sasa, pasia kwake Gyan, faulo, inapigwa kuelekea Njombe
Dak ya 25, Njombe wamefanya shambulizi moja kwa kupiga shuti kali lakini linakwenda nje, Simba wanaanza
Dak ya 24, Unarushwa tena kuelekezwa Simba, rusha pale unamkuta Okwi, kwake Nyoni, anajaribu kumtafuta Kapombe lakini unatoka nje, unarushwa kuelekea Simba
Dak ya 23, Njombe wanarusha, unatoka tena, unaelekezwa Simba
Dak ya 22, Mpira unarushwa kuelekea Njombe, wanarusha Simba, kwake Juuko, unatoka nje tena
Dak ya 21, Shiza Kichuya anashindwa kumalizia vizuri nafasi aliyotengenezewa na Gyan kwa mpira wa krosi na kwenda nje
Dak ya 20, Njombe wanashindwa kutumia vizuri nafasi ya kufunga, ilikuwa ni nafasi nzuri ya kusawazisha

Dak ya 19, Njombe wanarusha mpira sasa, baada ya Simba kuutoa
Dak ya 17, Hatari pale goooooooli, Bocco anaipatia Simba bao la kwanza, lilikuwa ni shuti kali alilopiga nje ya eneo la 18 

Dak ya 16, Okwi anakwenda na mpira kulia mwa Uwanja, hatari pale anajaribu kupiga chenga lakini anateleza
Dak ya 15, Mustafa Bakari anajaribu kupenya ngome ya Simba lakini mabeki wanakuwa imara
Dak ya 14, Njombe Mji wanapandisha mashambulizi langoni mwa Simba, Gyan anatoa nje
Dak ya 3, Simba wameonekana kuanza kwa kasi dakika hizi za mwanzo wakijaribu kusaka goli la mapema
Dak ya 2, Okwi anakosa nafasi ya kufunga bao la mapema. Alipata nafasi akiwa yeye na golikipa
Dak ya 1, Mpira umeshaanza Uwanja wa Sabasaba

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic