April 3, 2018



Na George Mganga

Mwandishi na Mchambuzi wa Soka, Edo Kumwembe, ametoa maoni yake kuhusiana na ubowa wa Uwanja wa Sabasaba ambao una kibarua hivi sasa kati ya Njombe Mji FC dhidi ya Simba SC.

Edo ameeleza kuwa Uwanja huo hauna ubora wa kuridhisha kwa kusema kuwa haustahili kupewa hadhi ya kuchezea mechi za ligi.

"Simuoni Okwi. Well Watanzania tusiwe wajinga...tuna ushabiki wa kijinga sana wa Mpira...tuwageukie wanaotuongoza... Huu uwanja hauwezi kuwa wa Ligi kuu... Pitch bovu na halitoi matokeo halali...mchezaji Kama Okwi hawezi kudrible hata hatua sita...Mechi inazungumzwa saaana katika media lakini ukienda uwanjani ni upuuzi tu... Nakerwa na pitch mbovu.. Hazitupi hadhi za mechi ya Ligi kuu" ameandika Edo kupitia Facebook.

 

3 COMMENTS:

  1. Humuoni Okwi.....Well ila kumbuka katika mechi nyingi za mikoani Okwi hajaonekana sana. Kiukweli timu zote hazikuweza kupata fursa ya kufanya kile kinachowezekana. Umeona hata golie David Kisu kafungwa goli zote kutokana na tatizo la Uwanja. La kwanza kafungwa mpira ulidunda wakati tayar karuka..la pili mabegi wamekwenda mpira umedunda umewapita miguuni. Kikubwa ni TFF kufanya kile kinachotakiwa kufanya na chama cha mpira wa miguu. Nahisi kama CCM inataka kuendelea kuingiza pesa kutokana na viwanja vyake inabidi kuvirekebisha. Niliona kiongozi nahic wa mkoa sijui ni Mara au Musoma huwa inanichanganya nae kahaidi Biashara itatumia uwanja ule wanaotumia.

    Nafikili imefika muda sasa kila timu inayotakiwa kupata leseni ni lazima iwe na Uwanja wake. Si lazima kiwe kikubwa sana...wawe na hata kama cha Azam kinatosha

    ReplyDelete
  2. Ni kweli katika eneo ambalo tuna fail sana basi ni viwanja vibovu na waamuzi. Juhudi za makusudi zinatakiwa katika maeneo Haya mawili.

    ReplyDelete
  3. ni aibu uwanja wa njombe kutumika ligi kuu jamani

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic