Matola alieleza kushangazwa na Simba kucheza chini ya kiwango kitu ambacho ni tofauti na namna timu hiyo ilivyoanza harakati za kuwania ubingwa mwanzoni mwa msimu wa ligi.
Kocha huyo alisema Simba ilicheza tofauti na michezo mingine na kujikuta akijiuliza haswa tatizo lilikuwa ni nini.
Akizungumza bada ya mchezo kumalizika, Matola alisema vilevile timu yake ilicheza vizuri zaidi ya Simba na ilipata nafasi nyingi ingawa ilishindwa kuzitumia kufunga magoli.
Katika mechi hiyo iliyopigwa mjini Iringa kwenye Uwanja wa Samora, mabao ya Adam Salamba kwa Lipuli na Laudit Mavugo kwa Simba yaliufanya mchezo umalizike kwa sare hiyo ya 1-1.
0 COMMENTS:
Post a Comment