April 22, 2018



Na George Mganga

Uongozi wa Yanga umeonesha nia za dhati kuwa bado unamhitaji Kocha George Lwandamina ili kuendelea kuinoa timu hiyo.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano wa Yanga, Hussein Nyika, amesema bado wanafanya jitihada za kumrejesha Kocha huyo aliyeondoka kimyakimya kurejea kwao Zambia.

Nyika amesema Lwandamina ana mkataba na Yanga hivyo bado ni Kocha wao hivyo watajitahidi kadri wawezavyo waweze kumrejesha.

"Lwandamina bado ni Kocha wetu na ana mkataba na timu, tunajitahidi kadri tuwezavyo ili tuweze kumrudisha" alizungumza kupitia kipindi cha Spoti Leo cha Radio One.

Yanga imezidi kumpigania Kocha huyo ili arejee kuja kukiongoza kikosi cha Yanga ambacho kipo katika mashindano ya kimataifa hivi sasa, vilevile kikiwa na mechi kadhaa zilizosalia kwenye ligi.




1 COMMENTS:

  1. Yanga msiogope nynyi mtashinda tu bila ya kocha

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic