MECHI YA WATANI WA JADI SHUGHULI NZIMA KUANZA SAA MBILI, NI KWA MTINDO HUU
Mechi ya Ligi Kuu Bara ambayo inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchi kati ya Simba na Yanga Aprili 29 2018 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, unaambiwa shughuli nzima itaanza saa mbili.
Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limesema kuwa Uwanja wa Taifa utafunguliwa kuanzia saa mbili asubuhi ili kutoa nafasi kwa watu kuingia.
Aidha TFF imesema itaimalisha ulinzi wa nguvu ikiwemo kufungwa kwa Camera zaidi ya 100 ili kurekodi matukio mbalimbali yatakayokuwa yanafanyika Uwanjani.
Mechi hiyo inayowakutanisha watani wa jadi huwa ni ya aina yake na huteka hisia za mashabiki wengi wa timu hizo za Kariakoo.
Vikosi vyote vya Simba na Yanga viko mjini Morogoro hivi sasa vikijiandaa na mchezo huo utakaopigwa Jumapili ya wiki hii.
0 COMMENTS:
Post a Comment