MKONGO WA YANGA AJA NA MFUMO MPYA
Kocha Mkongomani wa Yanga, Mwinyi Zahera, jana alikiongoza kwa mara ya kwanza kikosi cha Yanga kujifua zikiwa zimesalia siku chache kabla ya kuvaana na Simba.
Zahera aliwasili mjini Morogoro jana ili kukiona kikosi hicho baada ya kumalizana na uongozi wa Yanga kuhusiana na masuala ya kuanza kazi.
Zahera aliingia na mtindo mwingine katika mazoezi ya Yanga kwa kuwaongoza wacheza kucheza mpira kwa spidi huku akiwasisitiza wasipoteze pasi.
Mkongo huyo aliweka msisitizo huo wa kutopoteza pasi ili kumnyima nafasi adui ya kuchukua mpira.
Licha ya kuanza kukinoa kikosi hicho jana, Uongozi Yanga umesema bado hajaanza kazi rasmi kutokana na kufuatilia kibali chake cha kazi.
Labda atajaribu kuniridhisha kwa mfumo huu..mimi huwa sipendi pass za mwendo wa taratibu na watu wengine wakiwa wanatembea ndani ya Uwanja. Nataka timu ishambulie na pass za haraka. Sasa kocha huyu kama ataweza kuuweka na wachezaji wakawa na uharaka wa kuufanyia kazi nahc timu itafanya vizuri kwenye mechi za kimataifa. Hii mechi ya jumapili hainaga mwenyewe..ni mechi za wakubwa...huwezi kuzitabilia
ReplyDelete