Simba itakuwa mwenyeji katika mpambano huo ulio na shauku kubwa kutoka kwa mashabiki na wadau wa soka la Tanzania.
Mkude ameeleza kuwa Simba wanahitaji kupambana ili kupata alama tatu muhimu zitazowafanya wazidi kutengeneza mazingira ya kuutwaa ubingwa wa ligi msimu huu.
“Mechi yetu na Yanga ni ngumu kwa sababu kila mmoja anajua ukubwa wa mchezo wenyewe ambao mara nyingi huwa na ushindani.
“Kikubwa tunachotakiwa kukifanya ni kupata sapoti na ushirikiano baina ya wachezaji katika mchezo huu ambapo uwezo wa timu kwa jumla ndiyo utakaoamua ushindi,” alisema Mkude.
0 COMMENTS:
Post a Comment