April 26, 2018



Kuelekea mechi ya watani inayosubiriwa kwa hamu nchini na wapenzi wa soka, klabu za Yanga na Simba zinaendelea na mazoezi leo mjini Morogoro.

Timu hizo kongwe za Kariakoo zimeweka kambi mjini humo kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa ligi utakaopigwa jijini Dar es Salaam Aprili 29 2018.

Simba wanafanyia mazoezi yao kwenye Uwanja wa Jamhuri wakati Yanga wakiwa Chuo cha Biblia.

Ni siku siku tatu pekee zimesalia kuelekea kupigwa kwa kipute hicho kitakachotoa timu yenye dalili ya kuchukua ubingwa wa ligi msimu huu.

Simba ina alama 59 kileleni kwenye msimamo wa ligi na Yanga ikiwa imejikusanyia pointi 48 mpaka sasa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic