April 9, 2018




Pamoja na kutopewa nafasi kubwa, beki wa kati wa Yanga, Abdallah Shaibu 'Ninja', juzi Jumamosi alifanikiwa kumdhibiti kabisa mshambuliaji tegemeo wa Wolaita Dicha,  Mtogo, Arafat Djako na kushindwa kufanya chochote huku akipiga mipira 11 ya vichwa mbele yake.

Ninja ambaye amejiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Taifa Jang'ombe ya Zanzibar, juzi alicheza mechi yake ya kwanza ya kitamaifa tangu ajiunge na timu hiyo kutokana na kushindwa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza, akiishia kukaa benchi na wakati mwingine jukwaani.  

Katika mchezo huo wa Kombe la Shirikisho Afrika uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 ambapo beki huyo alicheza kwa umakini mkubwa, akiziba pengo la beki tegemeo wa timu hiyo, Kelvin Yondani ambaye hakucheza kutokana na madai ya kuwa na kadi mbili za njano.

Beki huyo katika kipindi cha kwanza, alifanikiwa  kuondoa mipira ya juu katika eneo la hatari kwa kupiga vichwa vitano na kipindi cha pili alipiga sita huku akiokoa mpira katika eneo la 18 mara tisa kipindi cha kwanza na mara 11 kipindi cha pili, ikiwa jumla yake ni 20 licha ya kutembea wakati wote na Mtogo wa Dicha.

Mara baada ya mchezo huo, Mkurugenzi wa Ufundi wa Dicha, Habtamu Hailemichael, amesema: "Yanga ni nzuri, hata ukiangalia safu yao ya ulinzi iliweza kuzuia tusipate mabao kutokana na kucheza kwa ushirikiano mzuri, sijui itakuwaje kwenye mchezo wa marudiano.”

Yanga inatarajiwa kurudiana na Wolaita Dicha, Aprili 18, mwaka huu kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Hawass uliopo kwenye Mji wa Hawass nchini Ethiopia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic