Katika kuelekea msimu wa kombe la Dunia 2018, Kampuni ya MultiChoice Tanzania kupitia king’amuzi chake cha DStv imezindua kampeni mpya ifahamikayo kama DStv ni moto! Mteja wa DStv sasa anaweza kujiunga na huduma iitwayo “DStv Now” na kutazama vipindi vya DStv wakati wowote mahali popote ikiwa ni pamoja na kupata fursa ya kuunganisha vifaa vitano (5) zaidi ikiwemo simu ya kiganjani, Tablet, Laptop au Desktop pamoja na Runinga.
Hii inamaanisha watu wa tano (5) tofauti wanaweza kutazama huduma ya DStv kupitia vifaa vitano (5) tofauti kwa wakati mmoja na kwa akaunti moja tu ya malipo ya mwezi!
Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaa Jana, Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania, Alpha Mria alisema “Wakati tunaelekea kwenye mashindano makubwa kabisa ya soka Duniani yaani Kombe la Dunia la FIFA , tunampa fursa mteja kutazama huduma ya DStv kwenye vifaa hadi vitano kwa wakati mmoja







0 COMMENTS:
Post a Comment