RUVU SHOOTING WASEMA MVUA YA JANA ILIWAOKOA AZAM FC, WALIPASWA KULA BAO NNE LAKINI
Na George Mganga
Uongozi wa Ruvu Shoting kupitia kwa Msemaji wa klabu hiyo, Masau Bwire, umesema kuwa mvua iliyonyesha jana imewaepusha Azam na kipigo.
Masau ametamba kuwa ilikuwa lazima wafe kwa jumla ya mabao manne lakini kutokana na mvua kunyesha kisha kusababisha Uwanja wa Mabatini kujaa maji, uliwaokoa Azam na kichapo hicho.
"Azam walitakiwa kufa nne leo, unajua hii mvua kama imewaokoa na kichapo, leo wajiandae kukipokea kwani bado kipo palepale. Tuna morali ya kutosha na tumejipanga vizuri" amesema Bwire.
Mechi hiyo iliahirishwa jana kufuatia mvua kubwa kunyesha na kusababisha Uwanja kujaa maji hivyo ilibidi uahirishwe na utafanyika tena leo mjini Mlandizi.
Azam FC itakuwa mgeni wa Ruvu Shooting ikiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa imejikusanyia alama 45 huku wapinzani wao wa leo Ruvu wakiwa nafasi ya 10 na alama 26.








0 COMMENTS:
Post a Comment