April 13, 2018



Na George Mganga

Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga, Charles Boniface Mkwasa, amesema kuwa timu zilizosalia katika mashindano ya Kombe la FA, haziko vizuri kiuchumi.

Kwa mujibu wa kipindi cha Michezo kupitia Radio One, Mkwasa ameeleza kuwa timu zote ambazo zimeingia hatua ya nusu fainali, hazina uwezo kwa kugharamika haswa katika suala zima la kusafili kwenda nje ya nchi kushiriki mashindano ya kimataifa.

Kauli hiyo imekuja kutokana na uwakilishi wa mshindi wa Kombe la Shirikisho kupewa nafasi ya kushiriki mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika, huku Bingwa wa ligi akishiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mbali na kushindwa kujikimu kifedha, Mkwasa amesema pia timu hizo hazina uzoefu na mashindano ya kimataifa hivyo zitakuwa zinashiriki mara ya kwanza.

JKT Tanzania, Singida United, Mtibwa Sugar na Stand United ndizo timu zilizoingia hatua hiyo ya mashindano ya Kombe la Shirikisho zikisubri kucheza mechi za nusu fainali.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic