April 23, 2018



Uongozi wa Singida United umefurahia kuingia hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho baada ya kuifunga JKT Tanzania kwa jumla ya mabao 2-1 katika Uwanja wa Namfua, mjini Singida, leo lakini ukisema hauhusiki na masuala ya kanuni.

Singida United imetinga hatua hiyo katika muda wa nyongeza 'Extra Time' kufuatia dakika 90 kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Mkurugenzi wa klabu hiyo, Festo Sanga, amesema kuwa wao wamefuraha kutinga hatua ya fainali ambapo watakutana na Mtibwa Sugar tarehe pili ya June 2018.

Aidha, Sanga amesema masuala ya kubadilika kwa kanuni wao hawasuki nayo bali wanajali kupata matokeo akieleza hilo linahusika na TFF na si Singida United.

Akihojiwa na Radio EFM kupitia kipindi cha michezo kuhusiana na kuongezwa kwa dakika 30 baada ya zile 90 kumalizika, Sanga ameeleza hawezi zaidi kuzungumzia hilo na wanachoangalia hivi sasa ni kujipanga dhidi ya Mtibwa kwenye fainali.

"Mimi siwezi kuzungumzia masuala ya kanuni kwasababu hayatuhusu, tnachoangalia kwa sasa ni namna gani tutajipanga kueleka mchezo wa fainali dhidi ya Mtibwa, hayo ya kanuni TFF wanahusika" amesema Sanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic