April 23, 2018



Na George Mganga

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetolea ufafanuzi kuhusiana na kuongezwa kwa dakika thelathini za muda wa nyongeza baada ya dakika 90 kukamilika kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho.

Hatua hiyo imekuja kutokana na mchezo wa hatua ya nusu fainali uliopigwa leo kati ya JKT Tanzania dhidi ya Singida United kuongezewa muda wa dakika 30 badala ya kupigwa matuta baada ya dakika 90 kumalizika kwa mabao 1-1.

TFF imetanabaisha kanuni kuwa zilibadilika ambapo hivi sasa zinaeleza kuwa endapo timu zitatoka sare kwenye raundi ya kwanza mpaka ya sita, mshindi atapatikana kwa kupigiana penati tano kwa tano.

Na endapo zoezi la upigaji wa penati hizo tano halitatoa mshindi, zoezi la upigaji wa matuta litaendelea mpaka pale mshindi akipatikana.

Aidha, kanuni hizo zinaeleza kuwa kuanzia hatua ya robo fainali, timu zikimaliza dakika 90 bila mmoja kupata matokeo, iwe suluhu ama sare ya mabao yoyote ile, dakika 30 za nyongezwa zitatumika kutafuta mshindi wa mchezo huo.

Endapo pia dakika 30 zilizoongezwa hazitapata mshindi, hatua itakayofuata ni ile ya upigaji wa penati tano kwa tano mpaka pale mshindi atakapopatikana pia.

2 COMMENTS:

  1. Mmmmh,kaz tunayo hpa tunaona yanga alinyimwa hki kila anaeingia tff hana jipya bora tenga arudi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic