Kuna taarifa taarifa zinasambazwa mitandaoni kwamba Ibrahim Ajibu, Gadiel Michael na Rafael Daud wametoweka kambini Morogoro ambako Yanga inajiandaa na mchezo wake dhidi ya Simba, Jumapili.
Inaelezwa tarifa hizo zimeandikwa na Bloig namba moja ya michezo nchini ya Salehjembe, jambo ambalo ni uzushi wa hali ya juu.
Hatuna taarifa hiyo na wala hatujaiandika leo wala siku yoyote na kwa wasomaji wetu wanaweza wakawa shahidi kwetu kwamba hatujawa na taarifa kama hiyo.
Tunawaomba wasomaji wetu kuipuuza kwamba haijaandikwa na SALEHJEMBE BLOG lakini TUWAONYE wapuuzi wanaochukia hatua tunazopiga kwamba waache uzushi na kutuhusisha na taarifa zisizokuwa na ukweli.
Huu ni ujinga na upungufu wa mawazo chanya kuhusiana na taaluma lakini pia kuhusiana na ubora wa matumizi ya mitandao.
Tuwaombe radhi wasomaji wetu kwa usumbufu wowote walioupata na kuwasisitiza kwamba chochote wanachokiona wanaweza kuthibitisha kwa kuingia kwenye blog yao ya www,salehjembe.blogspot.com
TAARIFA HIYO YA KIZUSHI HIII HAPA…
IBRAHIM AJIBU,RAFAEL DAUD NA GADIEL MICHAEL WATOWEKA KAMBINI YANGA MJINI MOROGORO
SALEH JEMBE / 3 minutes ago
Wakati Yanga wakiwa kambini mjini morogoro wakijiandaa na mchezo wao muhimu wa ligi kuu dhidi ya mtani wao Simba utakaofanyika tarehe 29/4/2018 siku ya jumapili katika uwanja wa Taifa jijini dar es salaam.
Wachezaji wake watatu muhimu kwenye kikosi hicho wametoweka kambini hapo bila taarifa baada ya kutoka mazoezini jioni hii wakijiandaa na mchezo wao na simba wakiwa chini ya kocha wao msaidizi Shadrack Nsajigwa.
Taarifa rasmi ya kutoweka kwa wachezaji hao kambini humo haijafahamika bado ila jitihada zinaendelea kufanyika kwa benchi la ufundi la timu ya yanga pamoja na uongozi mzima ili waweze kujua nini tatizo la wachezaji hao kutoweka kambini humo.
Visit website
Wewe nawe ni mzushi mbaya sana unaandika habari za uongo na kuzikanusha mwenyewe kujipatia umaarufu. Katika block zote Salehe inaongoza kutengeneza uongo.
ReplyDeleteTaarifa hiyo ya wachezaji wa Yanga kutoweka kambini inawezekana kabisa imezushwa na Yanga wenyewe kama psychological warfare ili kuwapumbaza wapinzani wao wafikiri kuwa Yanga dhaifu,wanamatatizo kede wa kede na kuwafanya SIMBA wa bwetweke kiakili na kimwili kuzani kuwa wanakwenda kukabiliana na timu dhaifu.
ReplyDeleteIkiwa ni kweli, inawezekana hawajapewa hela yao
ReplyDelete