April 25, 2018




Kocha Mkongomani wa Yanga, Mwinyi Zahera ameanza mdogomdogo kukinoa kikosi cha Yanga, leo jioni.

Mazoezi ya yanga mjini Morogoro, yamefanyika kwenye Uwanja wa Highland na Zahera alionekana akisaidiana na Noel Mwandila na Shadrack Nsajigwa kutoa maelekezo kadhaa.

Wachezaji wa Yanga walionekana kuendelea na mazoezi huku wakifuata maelekezo yaliyokuwa yakitolewa.


Zahera aliwasili mjini Morogoro akitokea jijini Dar es Salaam, na muda mchache baadaye akaungana na wachezaji hao mazoezini.



Kocha huyo amejiunga na Yanga kuchukua nafasi ya George Lwandamina raia wa Zambia ambaye aliamua kurejea kwao kwa madai ya kutolipwa mishahara yake.

Yanga ipo mjini Morogoro kambini kujiandaa na mchezo dhidi ya Simba ambao sasa ndiyo vinara wa Ligi Kuu Bara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic