Na Saleh Ally
Kila shabiki ana lake leo na wengi wanamini timu yao ndiyo itaibuka na ushindi lakini hoja zao wanazoziamini zinaminywa na takwimu.
Kama utaangalia ligi nzima, basi Simba ina nafasi ya kushinda kwa mambo mengi na ilipo sasa.
Lakini kama utaangalia mechi nane zilizopita, inaonekana mchezo ni mgumu na Yanga inaweza kuwa na nafasi ya kushinda kwa asilimia 5 zaidi.
Hivyo ni mchezo mgumu ambao unaweza kutoa 55% kwa Simba 45% kwa Yanga lakini bado kwa kutumia mechi nane zilizopita unaona Yanga ina 53% na Simba 47%.
Maana yake, ni mechi ambayo inakimbilia katika 50-50 na ugumu wake au ulaini utatengenezwa katika dakika 90 za leo pale Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Simba na Yanga kila upande umefanya vizuri katika mechi nane zilizopita Simba wakiwa wameshinda tano na tatu kutoka sare na Yanga wameshinda mechi sita na kutoka sare mbili mfululizo.
Kama katika dakika 720 Yanga wamefanikiwa kufunga mabao 20, hali ilivyo inaonyesha ni vigumu sana kuondoka bila bao angalau hata moja katika mechi moja.
Katika mechi nane zilizopita, Simba imeruhusu difensi yake kufungwa mara 7. Hii inaonyesha safu yao ina makosa madogo mengi na wanapaswa kuwa makini.
MECHI 8 KABLA YA LEO
YANGA:
- Lipuli 0-2 Yanga
-Yanga 4-0 Njombe
-Yanga 4-1 Majimaji
-Ndanda 1-2 Yanga
-Yanga 3-0 Kagera
-Yanga 3-1 Stand
-Yanga 1-1 Singida
-Mbeya 1-1 Yanga
SIMBA:
-Mwadui 2-2 Simba
-Simba 5-0 Mbao
-Simba 3-3 Stand
-Njombe 0-2 Simba
-Mtibwa 0-1 Simba
-Simba 3-1 Mbeya
-Simba 2-0 Prisons
-Lipuli 1-1 Simba
0 COMMENTS:
Post a Comment