Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji wa mashindano ya mchezo wa kujihami Tae kwo-ndo kwa nchi za Afrika Mashariki yanayofanyika Mei mwaka huu.
Rais wa Tae kwo-ndo kwa nchi za Afrika Mashariki, Kennedy Said alisema jana kuwa maandalizi ya mashindano hayo yameanza.
Alisema mashindano hayo yatakutanisha wachezaji zaidi ya 70 kutoka nchi za Uganda, Burundi, Kenya, Rwanda na wenyeji Tanzania.
Kennedy ambaye pia ni Rais wa Tae Kwo-ndo Tanzania alisema zimealikwa nchi za Ethiopia na Sweden kushiriki mashindano hayo na zawadi mbalimbali zimeandaliwa kwa ajili ya washindi.
Kennedy alisema Tanzania ilipata nafasi ya kuchaguliwa kuwa mwenyeji wa mashindani hayo kutokana na mkutano wa nchi saba wanachama uliofanyika Kampala,Uganda Desemba mwaka jana.
Alisema washindi wa mashindano hayo watapata nafasi ya kushiriki fainali ya kuwania ubingwa wa mchezo huo Afrika utakaofanyika Addis Ababa, Ethiopia Agosti mwaka huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment