April 5, 2018





Suala la kiungo mshambuliaji, Mohamed Salah acheze au la katika mechi ya Merseyside Derby, linabaki kwa Kocha Jurgen Klopp.

Wengi walitamani kumuona Salah akicheza mechi hiyo dhidi ya Everton wikiendi hii lakini Klopp atajaribu kuangalia kwamba amchezeshe au kumpumzisha ili awe fiti zaidi watakapoivaa Manchester City katika mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Salah aliumia mguu katika mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya City akiwa amefunga bao moja na Liverpool kushinda 3-0.

Baada ya vipimo leo asubuhi, madaktari wamemruhusu kwamba anaweza kumtumia ingawa suala la kupumzika nalo, linaonekana kuwa ni sahihi zaidi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic