April 11, 2018




Baada kuwadhibiti Waethiopia, beki wa kati wa Yanga, Abdallah Shaibu 'Ninja' ameibuka na kusema kuwa  licha ya kucheza vizuri katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Wolaita Dicha, lakini bado anaona hajafikia kwenye kiwango chake.

Kumbuka pamoja na Ninja kuamini hajafikia kiwango chake lakini leo ameanza kuonyesha cheche kwa kufunga bao dhidi ya Singida United.

Katika mchezo uliochezwa Jumamosi iliyopita ambao ni wa kwanza wa kimataifa kwa beki huyo tangu ajiunge na Yanga msimu huu kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Taifa Jang’ombe, Ninja alifanikiwa kumdhibiti mshambuliaji hatari wa Dicha, Mtogo, Arafat Djako na kushindwa kufanya chochote huku akipiga mipira 11 ya vichwa mbele yake.

Ninja amesema kuwa licha ya kucheza vizuri katika mchezo huo bado anaona hajafikia kiwango chake cha zamani huku akiwashangaa waliokuwa wakihisi angefanya vibaya kwenye mchezo huo.

"Kiukweli kwangu ni jambo kubwa kufanikiwa kucheza mechi ya kimataifa maana ndiyo ya kwanza, nashukuru imeweza kuniongezea vitu na kunifanya nizidi kuwa bora kwa sababu akili nyingi inatakiwa kuwadhibiti washambuliaji wao.

"Lakini nafahamu kwamba wapo waliohisi ningeweza kuharibu katika mchezo ule ila haikuwa hivyo kwa kuwa nilijipanga ingawa bado sijafikia katika kiwango changu ambacho nimekizoea siku zote," alisema Ninja.
Ikumbukwe, Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa wikiendi iliyopita kabla ya kuelekea Ethiopia katika mchezo wa marudiano ambao utapigwa Aprili 18, mwaka huu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic