April 11, 2018




Huku Mbeya City ikitarajiwa kuvaana na Simba kesho Alhamisi kocha mkuu wa timu, Ramadhan Nswanzurimo amefunguka kuwa wapo tayari kupambana na Simba lakini waamuzi wa mchezo huo ndiyo watakaoamu  hatima yao.

  Mchezo uliopita uliozikutanisha timu hizo pale Sokoine, Simba ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 huku  bao la Shiza Kichuya kwenye mchezo huo likizua utata kuwa lilikuwa ni la kuotea.

Kocha huyo alisema kuwa maandalizi yake ni mazuri na vijana wake kwa sasa wako kwenye moto hivyo wapinzani wajipange na pia waamuzi wanatakiwa kuwa makini kwenye mchezo huo.

“Tumejipanga vyema kabisa kupambana na Simba wachezaji wangu wako vizuri Simba ni timu kubwa ambayo tunaiheshimu lakini kwenye mchezo huo waamuzi ndiyo wataamua hatima yetu dhidi ya Simba.

“Sababu nakumbuka mchezo uliopita ilitupa shida sana kwa upande wa waamuzi tulipocheza na Simba na makosa mengine yalikuwa yakifumbiwa macho hivyo safari hii wanatakiwa kuongeza umakini kuhakikisha kila kitu kina kwenda sawa.

 “Hatuna hofu na Okwi sijui Bocco sababu vijana wangu kama wataendeleza moto kama ambao walionyesha mbele ya Azam basi Simba watakuwa na kazi ya ziada kwenye mchezo huo,”alisema Nswanzurimo.

SOURCE: CHAMPIONI

6 COMMENTS:

  1. Subiri zamu yako,mwenzako kanyolewa leo sasa wewe jitape utaona shuhuli kesho,achana na mfaransa wewe,ukisikia kichuya,bocco anakwenda kule OKWIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII,ujue tayari kimeshanuka.

    ReplyDelete
  2. Tena kesho mnapigwa na ASANTE KWASI.

    ReplyDelete
  3. Visingizio sasa imekuwa ni marefarii.Tatizo hizi timu zinapania mechi za Simba,Yanga na Azam na matokeo yakiwa sivyo waliyokuja nayo mfukoni basi lawama zote ni marefarii hawachezi kwa haki.
    Nilimshangaa msemaji wa Mtibwa Kifaru kulalamikia refarii ktk mechi ya Simba na Mtibwa kuwa refarii hakucheza kwa haki.Na wala sikumsikia goli alilofunga Boko na refa akalikataa.
    Timu zisiwe zinaingia kucheza mechi na akili ya refarii kuwa atapendelea.Wacheze mpira waache maneno

    ReplyDelete
  4. Mchezo wa mpira ni mchezo unachezwa hadharani na matokeo yake pia yapo dhahiri, kuanza kutoa visingizio kwa waamuzi ni kuwa na hofu na kujihami hivi kama washambuliaji wa team husika wanapo shindwa kufanya kazi yao leo utatupa lawama kwa wamuzi?? Simba ni club moja wapo kwa sasa wachezaji wake wana cheza kwa hofu kubwa wachezaji wa team pinzani wanawachezea rafu za makusudi kabisa. Mbeya City njooni uwanjani mkiwa mshajiandaa kupokea kipigo kutoka kwa Bocco.

    ReplyDelete
  5. mchezo utaamkuiwa na marefa? ebho kwani huwa unaamuliwa na nani?

    ReplyDelete
  6. Tumeshawazoea,safari hii hakuna kubebwa lazima kieleweke,kuna wanaosema simba hamuwezi mtibwa na ikitokea simba kamfunga mtibwa ujue kanunua game,sasa kwanini na nyie msinunue?yani kila kitu kizuri cha simba lazima mtakitia uharamu ilimradi tu,na safari hii mwakosa kote mwakani mtatembea kwa miguu kwenda ligi za mikoani,tena mumshukuru sana Lwandamina kufikia hatua yakusaidia club kwa mshahara wake,mtamkumbuka sana poleni.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic