VIJEBA KARUME BOYS WASABABISHA SERIKALI KUINGILIA KATI, YATOA TAMKO HILI
Kufuatia kuondoshwa kwa Karume Boys kwenye michuano ya CECAFA (U17) inayofanyika nchini Burundi hivi sasa kutokana na wachezaji wake 12 kuzidi umri, serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema itaanza uchunguzi juu ya suala hilo.
Kupitia Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mh. Omary Hassan, amesema watafanya uchunguzi kuwabaini wote waliohusika na kikosi hicho kuondolewa kwenye mashindano.
Hassan ameeleza kuwa ZFA imefanya makosa mpaka timu hiyo inapeleka vijana ambao wamezidi umri, kitu ambacho ni kinyume cha taratibu na mashindano.
Karume Boys imeondolewa kushiriki mashindano hayo huku ikifungiwa mwaka mmoja pamoja na faini ya dola za kimarekani, 15,000.
Mbali na Karume Boys, Ethiopia nayo iliondolewa kwenye mashindano hayo baada ya kubainika wachezaji wake kadhaa kuzidi umri nao wakilimwa faini ya dola hizo za kimarekani 15,000.
0 COMMENTS:
Post a Comment