April 17, 2018



Kikosi cha Yanga tayari kimekamilisha maandalizi ya mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Wolaita Dicha kuelekea mechi itakayopigwa kesho mjini Awassa, Ethiopia.

Meneja wa timu, Hafidh Saleh, ameeleza kuwa tayari kikosi kimeshakamilisha mazoezi yake leo na wako tayari kwa mtanange huo.

Akizungumza moja kwa moja kutoka Ethiopia, Saleh amesema wachezaji wote wako fiti kucheza kesho na akisema hakuna aliye majeruhi.

Yanga itasonga mbele kwenye mashindano hayo mpaka hatua ya makundi endapo itatoa sare yoyote ile ama kuibuka na ushindi.

Katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Dar es Salaam, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Kusonga mbele kwa Yanga kutaiwezesha kutwaa zaidi ya milioni 600 za kitanzania kama ilivyo utaratibu wa CAF kutoka kitita hicho cha pesa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic