May 5, 2018



Mjumbe wa Baraza la Wazee wa katika klabu ya Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali, ameilalamikia serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa imewafanya kuwa yatima.

Akilimali ameeleza kuwa serikali imesababisha Yanga kufikia mpaka hapo walipo huku akidai kuwa imewabana wasipate baba.

Akizungumza kupitia Spoti Leo ya Radio One Stereo, Akilimali ameeleza kuwa Yanga hivi inapitia wakati mgumu kutokana na namna hali ilivyo mbaya klabuni.

Mzee huyo ameigusia serikali kutokana na kuzuia mikutano kadhaa ya Yanga iliyopaswa kufanyika nyuma na mambo mengine huku akiilenga Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo iliyo chini ya Dkt. Harisson Mwakyembe.

Kauli hiyo imekuja kufuatia baadhi ya nyota wa Yanga ikiwemo Obrey Chirwa, Papy Kabamba Tshishimbi na Ibrahim Ajibu kusalia nchini wakati kikosi kikisafiri kuelekea Algeria kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger utakaopigwa kesho.

3 COMMENTS:

  1. Sasa Mzee ulitaka serikali waifanyie ni yanga, iwalipie madeni au waliogoma serikali iwalazimishe kujiunga? Mini naamini matatizo ya yanga yanatokana na jinsi mlivokuwa mkiwafanyia maonevu simba kwa jinsi mlivokuwa mkiwanyanganya wachezaji wao nyota kwa kutokana na mapesa mliyokuwa nayo wakati ule. Unaambiwa unapopanda juu umsalimu uliyemkuta chini kwani wakati wa kushuka utamkuta tena.

    ReplyDelete
  2. Dah kwani Yanga ni klabu ya serikali? Kila siku mnaelezwa badilisheni mfumo wa uendashaji wa klabu angalau Simba imejifunza kidogo kuwa soka la sasa linahitaji pesa na kuipata hiyo pesa inabidi mifumo ya kibiashara na inayoeleweka.Lakini hawa wazee wamekuwa wabishi kubadili mfumo wa uendashaji klabu na wanasahau kuwa Yanga wameikuta na wataiacha.

    ReplyDelete
  3. Akilimali zile million 800 ulishazitumia?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic