May 28, 2018



Kikosi cha Azam kimelipiza kisasi kwa Yanga baada ya kuichapa mabao 3-1 leo katika mchezo kuhitimisha mechi za ligi kuu msimu huu uliopigwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.


Timu hizo mbili zilikuwa zinapambana kuwania nafasi ya pili ambapo Azam wamefanikiwa kutokana na ushindi huo.

Mabao ya Azam yametiwa kimiani na Yahya Zayd mnamo dakika ya 4, Shaaban Idd (60') na Salum Abubakar 'Sure Boy' (68').

Azam walijifunga na kuipa Yanga bao la kufutia machozi mnamo dakika ya 49 kupitia kwa Abdallah Kheri (49') kwa kichwa wakati akifanya harakati za kuokoa mpira.

Matokeo hayo yanaifanya Azam kulipiza kisasi baada ya kfungwa mzunguko wa kwanza kwenye dimba la Azam Complex kwa jumla ya mabao 2-0.

Vilvile Azam wamechukua nafasi ya Umakamu Bingwa kwa kufikisha alama 58 huku Yanga ikishika nafasi ya tatu ikijikusanyia pointi 52.

2 COMMENTS:

  1. Jamani imekuwa nyanya kiasi hicho,haifai jamani lazima hatua za kuikoa zifanyike kwani tunahitaj strong big four teams.

    ReplyDelete
    Replies
    1. MasiQini Yaaangaaa! :>) :>) :-) :-) [-( [-(. Yaan hadi wanatia huruma. Duuh! Kweli hujafa hujaumbika

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic