Kiungo wa klabu ya Azam FC, Salum Abubakar 'Sure Boy' ametamba kwa kueleza kuwa watajipanga vizuri kuelekea msimu ujao wa ligi ili waweze kuchukua ubingwa.
Sure Boy ameshindwa kulibeba taji la ligi msimu huu baada ya timu yake kumaliza ligi ikiwa nafasi ya pili kwa kujikusanyia pointi 58 na Simba ambao ni mabingwa wakiutwaa kwa kufikisha alama 69.
Kauli hiyo ameizungumza mapema baada ya mchezo dhidi ya Yanga kumalizika waliofanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1.
Kiungo huyo alifanikiwa kufunga bao lake la kwanza msimu huu likiwa la tatu mnamo dakika ya 68 na kufanya matokeo yamalizike kwa 3-1.
Mara ya kwanza na mwisho Azam kuchukua ubingwa wa ligi ilikuwa ni msimu wa 2013/14 iliomaliza bila kufungwa mechi hata moja.








0 COMMENTS:
Post a Comment