BAADA YA KUCHUKUA UBINGWA BILA KUFUNGWA, SIMBA WATAKA KUTENGENEZA REKODI NYINGINE, HII HAPA
Na George Mganga
Mbali na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara wakiwa na mechi tatu mkononi baada ya Yanga kupoteza dhidi ya Tanzania Prisons, Uongozi wa Simba umedhamiria kumaliza ligi bila kufungwa.
Simba imefanikiwa kuibuka na ushindi katika mchezo wa jana uliopigwa Uwanja wa Namfua mjini Singida dhidi ya wenyeji Singida United kwa bao 1-0 lililofungwa na Shomari Kapombe.
Baada ya ushindi huo, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, alisema kuwa kwa sasa wanapambana kumaliza ligi bila kupoteza mchezo wowote ili kuweka rekodi ya pili.
Manara alieleza hayo kutokana na timu hiyo kusaliwa na michezo miwili dhidi ya Kagera Sugar watakayoikaribisha Uwanja wa Taifa na baadaye watasafiri kuelekea mkoani Ruvuma Stadium kucheza na Majimaji FC.
Simba walifanikiwa pia kumaliza ligi bila kupoteza ikiwa ni msimu wa 2009/10 wakati Patrick Phiri akiwa Kocha Mkuu wa kikosi hicho na kufanikiwa kuutwaa ubingwa.
Kama Simba wakishindwa kuruhusu kupoteza mchezo hata mmoja kati ya miwili iliyosalia watakuwa wametengeneza rekodi hiyo kwa mara ya pili.
Walioihama nyumba ya Msimmbazi nawashauri warejee kabla ya kutoweka viwango vyao. Rejeeni nyumba imenona. kwani vijana mliowawacha kwa sasa wanayangoja mamilioni yao
ReplyDeleteNafikiri niwakati wa simba kujipanga zaidi kimataifa nasikusubiri dirisha la usajiri.wafanye skauti ya kutosha mapendekezo ya mwalimu
ReplyDelete