Bodi ya Ligi Tanzania, imetangaza kumsimamisha beki wa Yanga, Kelvin Yondani kutokana na kuonekana katika video akimtemea mate beki, Asante Kwasi.
Mtendani wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura amezungumza hivi punde na kusema suala lake limepelekwa Kamati ya nidhamu baada ya kuonekana haliwezi kusikilizwa na Kamati ya Saa 72 iliyokaa.
"Kwa hiyo sasa tunamsimamisha hadi hapo kamati itakapokaa na kuamua kuhusiana na suala lake," alisema Wambura.
Katika picha ya video ilimuonyesha Yondani akimtemea Kwasi raia wa Ghana katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyowakutanisha watani wa jadi, Yanga na Simba ambao walishinda kwa bao 1-0.
Suala hilo lilizua mjadala mkubwa miongoni mwa wadau, wakiwemo waliomtetea Yondani na walioona haikuwa sahihi.

Asanteni sana! mimi ukweli kitendo kile kilinikera sana na ulionesha ni kiasi gani mechezaji kama yeye alikuwa hajitambui. Uzuri ni kwamba ameona kiwango chake kinaishia hapahapa bongo. Niliona, kwasi akimlalamikia mwamuzi na mwamuzi yule hakufanya chochote. Kisha nikamuona Nicholas Gyan, kijana mdogo kutoka Ghana akimutuliza kwasi kwa ukomavu wa hali ya juu. Ebu wachezaji wa bongo tujifunze kwa hawa watu. Wanavitu wamekuja kutufunza licha ya kuwa viwango vyao ni kama vyenu.
ReplyDeleteJee kusimamishwa huko ina maana hata hiyo safari ya Al Jeria hatokuwemo? Jamaa wanajivuruga kwa njia haijawahi kutokea. Nini wanakitaraji huko uarabuni na kwani yale mamilioni hayakutumika kuwalipa wachezaji?
ReplyDelete98% ya TFF ni simba, sishangai kwa maaumuzi yao, lkn ikumbykwe Banda alipokuwa simba alipewa adhabu ya kufungiwa na TFF, lkn ilifutwa ili achezee timu ya Taifa, Leo Yondani anapewa adhabu wkt timu yake inaiwakilisha Taifa kwny mashindano ya kimataifa, huo ni uonevu na kuonyesha kutojali uwakilishi wa Yanga.
ReplyDelete