May 3, 2018





Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi (Kamati ya Saa) katika kikao chake cha Mei 1, 2018 chini ya Mwenyekiti wake, Clement Sanga ilipitia matukio mbalimbali ya Ligi Kuu ya Vodacom, na malalamiko ya klabu za Yanga na Arusha FC na kuyafanyia uamuzi.


Mechi namba 178 (Simba 1 vs Yanga 0).
Mchezaji Kelvin Yondani wa Yanga amesimamishwa hadi suala lake la kumtemea mate Asante Kwasi wa Simba katika mechi hiyo iliyochezwa Aprili 29, 2018 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam litakaposikilizwa na Kamati ya Nidhamu ya TFF.


Adhabu ya kusimamishwa imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 9(5) ya Ligi Kuu kuhusu Usimamizi wa Ligi.

4 COMMENTS:

  1. Kupitia vipengele vya sheria nakutoa tamko kulingana na sheria inavyotaka mpaka kamati ya nidhamu?amakweli kazi ipo hapo,haya acha tuangalie movie,tena hii ni season ya kikorea.

    ReplyDelete
  2. Nyosso huko kwote hakufikishwa hapo ni mahaba tu kweli pale Tff kuna miradi mingi ya watu. Hata Nyosso tunajua alikosa tu mtu wa kumpigania pale Tff ndio maana kipaji chake waliona aheri kiteketee Karia mfumo kuna siku utaondoka nae

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tatizo kuna kuleanaleana sana, thus why soka letu alifiki mbali..

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic