May 31, 2018



Kocha Zinedine Zidane ametangaza kujizulu kuifundisha soka klabu ya Real Madrid ikiwa ni siku chache baada ya kuipa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya.

Zidane ameeleza kuwa kuwa kila kitu kinahitaji mabadiliko hivyo ni wakati wa mtu mwingine kuingoza klabu hiyo yenye historia kubwa katika nchi ya Spain.

Kocha huyo amefunguka kwa kusema kuwa amefarijika kuwa mmoja kati ya waliofanikisha Real Madrid kutwaa mataji 13 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuweza kuwa sehemu ya historia hiyo.

Kocha huyo amesema Real Madrid inahitaji kuendeleza rekodi yake ya kufanya vizuri haswa kuzidi kupata matokeo katika michuano mbalimbali mikubwa.

"Kitu ninachokiwaza ni timu iendelee kupata matokeo, inahitaji kuwa na mabadiliko na inahitaji mtu mwingine, naipenda Real Madrid" amesema Zizou.

Zizou anaondoka Madrid akiweka historia ya kubeba taji la Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya mara tatu mfululizo na kuweka historia kubwa ndani ya Santiago Bernabeu.


2 COMMENTS:

  1. Manara atasema anakuja simba

    ReplyDelete
    Replies
    1. MasQini Mayeboo, ... hawakai wakaisha kuifikiria Simba. Simba wabbbbbayyaaa jamanii! ;(( Wamewafanyiza kitu mbaya Mayebo kiasi kwamba mawazo yao yote kila kukicha ni Taifa Kubwa tu. Mjitahidi kidogo, angalau mwakani tusikose wa kumtania. Mkiwa mdebwedoo ligi haitanoga. Ni aibu KMC kuja kuwa washindani wa Wekundu wa Msimbazi.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic