May 31, 2018


Beki wa Yanga aliyeripotiwa kupotelea kusikojulikana, Kelvin Yondani, ameonekana leo katika makao makuu ya klabu hiyo akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika.

Yondani ambaye alikuwa hapatikani kupitia simu zake za mkononi aliripotiwa kutokomea kusikojulikana huku akishindwa kuwa na kikosi cha Yanga tangu mchezo dhidi ya Simba uliopigwa Mei 29 2018.

Baada ya kuwasili kunako makao makuu ya klabu leo, taarifa zimeelezwa kuwa amefanya mazungumzo na Yanga ili kuweza kuongeza mkataba mwingine.

Ikumbukwe mkataba wa Yondani na Yanga unamalizika mwaka huu hivyo Nyika amefanya mazungumzo na beki huyo kuweza kuongeza ili aendelee kuitumikia klabu hiyo.




4 COMMENTS:

  1. Masikini roho yake

    ReplyDelete
  2. Kipi kilichomuondoa na kipi kilichomrudisha

    ReplyDelete
  3. Huruma . Kwani ana choice?

    ReplyDelete
  4. Ana shida gani? Huyu jamaa hakuwa hivi. Kamtemea mate Kwasi, akaigomea Yanga, akahusishwa kujiunga Simba, Ikasemekana kakubaliana na Azam na sasa karejea Yanga.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic