May 25, 2018





Wajumbe zaidi ya watano kutoka Shirikisho la Soka Afrika (Caf) na lile la Ulaya (Uefa) waliotua hapa nchini hivi karibuni kwa ajili ya kukagua miundo mbinu ambayo itatumika mwakani katika michuano ya vijana chini ya miaka 17 ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon), wameeleza kuridhishwa nayo.

Viongozi hao waliongozwa na  Mkuu wa Uhusiano wa Kimataifa wa Uefa, Eva Pasquier, Mwakilishi kutoka Caf, Junior Binyam ambao walikuwa na kazi ya kutembelea miundombinu mbalimbali ambayo itatumika kwa ajili ya fainali hizo mwakani.


Akizungumza na waandishi wa habari leo hii katika Hoteli ya Selena, Pasquier amesema: “Tuna wapongeze TFF kwa kile ambacho wamekifanya hadi sasa katika maandalizi ya kuelekea mashindano hayo. 

Tunashukuru kwamba tumekuta baadhi ya vitu viko vizuri kuanzia viwanja, hoteli, hospitali pamoja na miundombinu mingine zikiwa vizuri,” amesema Pasquier.

Kwa upande wake Binyam  amesema kuwa: “Tutahakikisha tutawasaidia Tanzania kufanya vizuri katika mashindano haya ya vijana kwa sababu hii ndiyo mara yao ya kwanza, tutashirikiana nao kwa kila sehemu. 

Hata hivyo, niwapongeze TFF kwa maandalizi ambayo wameshayafanya mpaka sasa,” amesema Binyam. 



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic