May 25, 2018




Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema walikuwa na asilimia mia ya kuifunga Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, lakini waliwaonea huruma kwa kuwa wako katika matatizo.

Yanga wamepata sare ya bao 2-2 dhidi ya Shooting katika mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara.


“Pale Jangwani kuna shida, kuna matatizo na mambo si mazuri. Tulipaswa kuwa na huruma.

“Tulifuata maandiko ya Mungu, anasisitiza huruma. Kama si hivyo, tungewapapaa Yanga kama ambavyo tulikuwa tumeahidi,” alisema.

Yanga inawania kupata nafasi ya pili ya Ligi Kuu Bara na inakwenda kukutana na Azam FC katika mechi ya mwisho.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic