May 24, 2018


Baada ya kuwabania Yanga kuwapatia mshambuliaji wao, Adam Salamba, uongozi wa Lipuli FC umetangaza kiasi cha fedha kwa klabu yoyote inayohitaji kumnyakua mchezaji huyo.

Taarifa zinaeleza kuwa Lipuli wanahitaji kiasi cha shilingi milioni 50 pekee ili kumuachia mchezaji huyo aliyekuwa kwenye fomu nzuri msimu huu.

Awali Yanga walituma maombi ya kumuhitaji Salamba kwa ajili ya kuwapiga tafu kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, lakini yaligonga mwamba kutokana na kanuni za TFF, CAF na FIFA kutoruhusu mchezaji kucheza zaidi ya timu mbili ndani ya msimu mmoja.

Inaelezwa kuwa klabu za Simba na Azam FC ndizo zilizoweka nia ya dhati kumsajili mchezaji huyo na mazungumzo yanaendelea mpaka sasa.

Wakati huo Yanga ambao walihitaji nia ya kuwa naye bado hawajazungumza chochote mpaka sasa kama wana lengo la kumsajili au la.


4 COMMENTS:

  1. Wasemavyo wahenga mwenye kisu kikali ndie atakae ondoka na sehemu kubwa ya nyama au kwa kifupi ndie atakaeondoka na nyama. Yanga walitaka kumchukua kiujanja ujanja huyu kijana kama akina khasan kesy Mungu bariki lipuli wameshtuka.

    ReplyDelete
  2. Hata Michael Katende wa Kagera Sugar kipindi hicho alitaka dau kubwa akaachwa sasa yuko wapi? Salamba anazihitaji zaidi Simba au Yanga kuliko timu zinavyomuhitaji yeye .

    ReplyDelete
  3. Ende kwa Mo kwenye uhakika

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic