May 5, 2018




Mastaa wa Yanga, Donald Ngoma na Amissi Tambwe, bado ni majeruhi na hawatarajii kurejea uwanjani hivi karibuni, sasa daktari mmoja mtaalam wa afya za wachezaji amefichua siri ya majeraha ya mastraika hao.

Siyo Ngoma anayesumbuliwa na misuli na Tambwe anayeumwa goti, pia Haruna Niyonzima wa Simba naye ni majeruhi wa muda mrefu akisumbuliwa na kifundo cha mguu.

Sasa Daktari Mwanandi Mwankemwa mtaalam wa afya za wachezaji pia ni daktari wa Azam FC, amesema kuwa, mastaa hao hawaponi haraka sababu wanaachwa binafsi kufanya mazoezi.

Mwankemwa alisema timu nyingi hapa nchini hazina makocha wa viungo, ndiyo maana nyota wengi wanachelewa kurudi uwanjani wanapopata majeraha.

“Mchezaji anapoumia halafu ukamuacha mwenyewe afanye mazoezi mepesi ili arejee kwenye kiwango chake kama zamani, utakuwa hautibu tatizo zaidi ya kumuongezea tu.

“Atakapokuwa anafanya hayo mazoezi bila ya kuwa na msimamizi kuna madhara yake kwa sababu anaweza kujiongezea dozi au kufanya kwa kiwango cha chini.

“Nitoe ushauri tu kwa timu zetu iwe Simba, Yanga au hata timu nyingine ziweze kuwa na kocha maalum kwa ajili ya mazoezi ya viungo ambaye atashughulika na wachezaji kama hao wanaotoka kwenye majeraha,” alisema Mwankemwa.

CHANZO: CHAMPIONI

1 COMMENTS:

  1. Simba wana kocha wa viungo waongelee hao yanga

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic