May 3, 2018



Na George Mganga

Afisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, ameliomba radhi Shirikisho la Soka Tanzania Bara (TFF) kupitia Bodi ya Ligi kufuatia kupewa onyo la kushangilia ndani ya Uwanja katika mechi dhidi ya Yanga.

Manara alishuka kutoka jukwaani na kuingia ndani ya Uwanja baada ya kushindwa kuvumilia furaha aliyokuwa nayo kutokana na Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara ameomba radhi kwa bodi ya ligi huku akieleza kuwa alipitiwa na mhemko baada ya furaha kuzidi.

Licha ya kuomba msamaha huo, Manara ameeleza kuwa hajajua Simba kama ikitwaa ubingwa hali ya furaha yake itakuwaje, yawezekana akaingia tena Uwanjani kushangilia na kucheza.



Mapema leo mchana Bodi ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi kupitia Mwenyekiti wake Clement Sanga ilitoa onyo kali kwa Manara, kuhusiana na kuingia uwanjani kushangilia ushindi wa timu yake baada ya mchezo kumalizika.

Kitendo cha kufanya hivyo ni ukiukwaji wa Kanuni ya 14 (11) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo, na adhabu dhidi yake imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

1 COMMENTS:

  1. Wamekosa kazi hao wameshindwa kumwadhibu aliyepiga kiwiko na kumtemea mate kwasi?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic