May 3, 2018


Mabingwa wa soka Tanzania, Yanga wameondoka nchini kwenda Algeria kuivaa USM Alger katika mechi ya Kombe la Shirikisho.

Mechi hiyo itapigwa Jumapili lakini Yanga wameondoka katika hali inayoonyesha hawakuwa na morali.

Jana kulikuwa na mgomo baridi wakidai malipo yao, lakini uongozi ukajitahidi kukanusha kwa kuwa kuna baadhi ya wachezaji wamegoma kuondoka na timu.

Kocha Mwinyi Zahera raia wa DR Congo naye alikuwa sehemu ya msafara huo pamoja na wasaidizi wake.






11 COMMENTS:

  1. Acheni story za kutunga, kama uongozi umekanusha we hizo habari umezipata wapi!?

    ReplyDelete
    Replies
    1. wajinga sana hawa vikaragosi wa kassim dewji,yani sijui wanachotaka nini,kuona yanga inakufa inabaki simba peke yake au

      Delete
  2. Lakini Yanga imekuwa ikikanusha kila kitu. Kwani ni uongo kuwa wachezaji hawajalipwa stahahaka zao kwa muda mrefu. Hao wachezaji namna wanavoonesha pichani ni kuwa wanyonge na uso chini

    ReplyDelete
  3. Kuwa mchezaji ni sawa na kuwa mwanajeshi ni muhimu kutanguliza uzalendo....

    ReplyDelete
  4. Hata habari za kuondoka kwa lwandamila uongozi wa yanaga ulikanusha. Kwa hivyo habari za wachezaji kugoma ni za kweli kabisa tusifiche maradhi.

    ReplyDelete
  5. Kwani unahc ni yanga tu ndio hawajawalipa wachezaji wao???timu zipo nyingi ila tunaangalia ukubwa wa story. Kwanini hawakuandika hilo jambo majuzi??wameandika leo kwasababu wamepata sababu...picha kupigwa kwenye "angle"..hiyo imepelekea kupata taswira la jambo la kutengeneza. Suala la Mishahara hata pale Champion unaweza kukuta watu wanadai malimbikizo yao ila sababu hakuna wa kuwafatilia hlio huwezi pata.
    Suala la malipo kwa mfanyakazi ni baina ya mfanyakazi na mwajiri wake..si suala linalomuhusu mtu mwingine. Yanga ni Taasisi inaweza kuchukua pesa popote kama mkopo na kuwalipa wachezaji chini ya mwamvuli wa TFF. Kama ni timu kudaiwa vioongozi wa Yanga watakuwa wazembe sana endapo wanaongoza Taasisi kubwa alafu wanakaa kimya. Timu zote hizi kubwa mbili wanashindwa kutumia vizuri madaraka ya kunufaisha timu zote na kuleta maendeleo zaidi ya kujinufaisha wao wenyewe. Angalia mfano wa timu "watani"...wanavyopata shida viongozi wao...unapata picha gani???hili suala lipo pande zote. We unahc hakuna mtu anaeweza kutoa pesa kwa ajili ya ujenzi wa viwanja katika hizi timu zetu???tatizo ni ujanja ujanja.

    ReplyDelete
    Replies
    1. tukiwaambia waandishi wa bongo vilaza hawana uzalendo wanakasirika,unaweza kuweka stori kwa style kwa timu inayokwenda ugenini ikiwakilisha nchi wewe ukiwa ni mwandishi wa nchi hii,unalo jukumu la kujaribu kuijenga timu kisaikolojia kwenye home media,habari na picha sampuli hii ungeacha yanga ikakutane nayo ugenini algiers sio wachezaji wanasoma media ya home ndani ya ndege wanaona habari na picha ya kuwashusha morali before hata hawajakanyaga ugenini,hivi hamjui kitu inaitwa media campaign kwenye mashindano ya kimataifa kwa media home kuandika habari in favor of home team and against the visiting team?saleh nimekudharau sana kwa kuweka usimba wako kwenye kila habari za yanga ili yanga iharibikiwe,unafeli bro

      Delete
  6. Kwanini hayajatajwa majina ya wachezaji kama ilivokuwa siku zote,au mara hii ni siri?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Chirwa ajibu kakolanya. Mpka hamtaka kipa kabwili abaki mazoez timu ya taifa

      Delete
  7. Kuwa mchezaji kama kuwa mwanajeshi, anasema Ndugu Polepole. Kwani wanajeshi nao hukaa miezi kadhaa bila ya kulipwa mishahara?

    ReplyDelete
  8. Kuwa mcheza mpira ni sawa tu na kazi nyingine yoyote....lazima wachezaji wapate stahiki zao kadri inavyotakiwa. Japo siungi mkono tabia ya mgomo, wachezaji wenye tabia hizi waondoshwe kwenye kikosi, mtu kama Chirwa nitashangaa kama wataendelea kumbakiza...uongozi Yanga mmeshindwa kudhibiti nidhamu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic