Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassan Dalali, naye amefunguka kwa kueleza kuwa hajafurahishwa na kitendo hicho alichofanya Yondani kwa kinashusha heshima yake ndani ya soka la Tanzania.
Kupitia Spoti Leo ya Radio One, Dalali ambaye aliwahi kuingoza Simba kwa mafanikio, amesema Yondani alikosea na si vema tukio kama hilo likajirudia kwani halipendezi hata kidogo.
"Kwakweli si kitendo kizuri, Yondani alikosea na si vema mambo kama haya yakifanyika kwa wachezaji wetu kwa maana hayapendezi hata kidogo" alisema Dalali.







Mimi inanistaajabisha kuwa hawezi kuchukuliwa hatua Simba ipeleke mashitaka na hapa inaonesha huu ni muelekeo mpya wa ajabu na kuchekesha.
ReplyDelete