MASHABIKI WAIPA NGUVU YANGA KOMBE LA SHIRIKISHO, NI AMSHA-AMSHA TAYARI KUWAMALIZA WAALGERIA
Wakati safari ya Yanga ikitarajiwa kuanza kesho kuelekea Algeria kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya U.S.M Alger, uongozi umesema mpaka sasa mashabiki wengi wamejitokeza kujiandikisha.
Kupitia Afisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, amesema kuwa kikosi kimeshapata nguvu kutoka kwa mashabiki wengi ambao tayari wameshajiandikisha kwa ajili ya safari hiyo.
Yanga ilitoa nafasi kwa mashabiki ambao wapo tayari kwenda kuipa hamasa timu yao na kuweka kiwango cha malipo ambacho kila mtu anapaswa kukitoa.
Mchezo huo wa mkondo wa kwanza utapigwa Mei 7 2018 huko Algeria.








Umuhimu kupata mashabiki wengi na mungu akipenda kombe la shirikisho litakuwa la Mkemi na Yonani mwaka huu
ReplyDelete