May 21, 2018

 



Wanachama wa Simba wameridhia na kupitisha muundo wa ubadilishwaji wa katiba ya klabu hiyo kutoka ule wa awali wa uwanachama kwenda kwenye mfumo wa hisa ambao unatumiwa na klabu kubwa duniani kama Manchester United ya England au Real Madrid ya Hispania.


Wanachama hao wamekutana leo katika mkutano wa dharura jijini Dar es Salaam na kuridhia kwa pamoja kuhudiana na hilo mbele ya viongozi na serikali.

Upande wa Serikali iliwakilishwa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe pamoja na Katibu Mkuu wa BMT, Mohammed Kiganja.

Mwekezaji ambaye tayari alijitokeza na kutangaza kuwekeza kwa Sh bilioni 20, atakuwa na nafasi ya hisa 49% na zinazobaki zinakwenda kwa wanachama na hiki ndicho serikali ilichokuwa inakisisitiza.


Hisa 51% zitauzwa kwa wanachama wa klabu hiyo na baadaye litaundwa kundi la watu nane kuwaongoza.

Maamuzi hayo ya kubadili muundo wa katiba ya Simba ulifikiwa na wanachama zaidi ya 1000 ambao walijitokeza kwenye mkutano mkuu wa mabadiliko ambao ulifanyika leo Jumapili katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwl Nyerere, Posta jijini Dar na kuendeshwa na Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’.


2 COMMENTS:

  1. Hongera sana Simba na wanasimba kwa kukamilisha suala hili la mabadiliko ya katiba. Mohamed Mo ni miongoni mwa wanasimba kindaki ndaki. Mengi yanaweza kusemwa juu ya uwekezaji wake pale SIMBA lakini kwa tunaemfahamu Mo ni dhahiri alichokiekeza Mo pale Simba ni Mapenzi yake zaidi. Hapana shaka yeyote SIMBA na Yanga ni Shamba la bibi kwa baadhi ya wasimamizi wa hizi timu. Na ndio maana kuna baadhi ya watu hawakuwa na hawatakuwa tayari kufurahia mabadiliko ya kuliona shamba la bibi likimilikishwa. Mo ni miongoni mwa wafanyabiashara mahiri na smart kwa hivyo tunaimani kubwa kabisa kwa kutumia elimu na uzoefu wake katika masuala ya uendeshaji kibiashara ataweza kuisadia SIMBA kujijenga kiuchumi. Ila Mo anapaswa kupewa ushirikiano wa hali ya juu kutoka kwa wadau mbali mbali wa mpira nchini. Kuja kwa Mo SIMBA ni habari nyengine njema kwa soka letu baada ya Baharesa kuwekeza Azam na hata kwa muekezaji wa Singida United. Kwa hivyo ni matarajio yetu watanzania kuona kasi ya kiwango cha soka letu kikikuwa. Hongera sana Simba. Pongezi sana Mo kwa kuonesha uzendo wako kwa klabu na nchi kwa ujumla. .

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic