May 6, 2018




Kocha wa zamani wa Manchester United, Alex Ferguson amefanyiwa upasuaji baada ya kugundulika ghafla ana ugonjwa wa ubongo ujulikanao kwa jina la subarachnoid haemorrhag.




Salehjembe imefuatilia ili kupata uhakika kwamba subarachnoid haemorrhag ni ugonjwa upi?


Subarachnoid haemorrhage si ugonjwa unaojulikana sana au unaowatokea wengi lakini ni aina ya “kupararaizi”.

Unatokana na mtu kupata tatizo la damu kuvuja ndani ya ubongo wake na ni moja ya ugonjwa hatari sana na rahisi kusababisha kifo.

Kwa Uingereza, takwimu zinaonyesha, Subarachnoid haemorrhages umewaandama si zaidi ya mtu mmoja kati ya 20 waliopooza.

Kawaida hauna tabia ya kuonyesha hali ya tahadhari, lakini wakati mwingine subarachnoid haemorrhage unaweza kuanza kunapokuwa na matukio ya kutumia nguvu kama mapigano au kubeba vitu vizito.


DALILI ZAKE:  
  • Kuumwa kichwa sana, maumivu yake hufanana na mtu aliyepigwa kichwani na kitu kizito.
  • Maumivu makali na shingo kukaza
  • Kujisikia mgonjwa na usijue unaumwa nini hasa
  • Kupata maumivu unapoangalia mwanga (photophobia)
  • Kuona “double double”, mfano kuona mtu mmoja wakiwa wawili
  • Viungo kutofanya vizuri, kushindwa kuzungumza vizuri na hata mdomo kwenda upande
  • Kuanza kutetemeka baadhi ya viungo vya mwili kama mkono, kichwa, mdomo na kadhalika

TIBA:  
Kama utagundulika kwamba unaweza kuwa ugonjwa huo, kitu cha kwanza ni vipimo na kama kunakuwa na uhakika, mara nyingi ni kupambana kuiondoa ile damu iliyo kwenye ubongo. Inaweza kuwa kwa dawa au upasuaji.

SALEHJEMBE

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic