KABWILI AREJESHWA NGORONGORO HEROES KWA MSAADA WA TFF
Kipa wa akiba wa klabu ya Yanga, Ramadhani Kabwili, amerejeshwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes.
Kwa mujibu wa Afisa Habari wa TFF, Clifford Mari Ndimbo, amesema kuwa kipa huyo amerejeswa kikosini na sasa ameungana na wenzake kambini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu AFCON (U20) dhidi ya Mali, Jumapili ya wiki hii.
Kabwili aliondolewa na kikosini na Kocha Ammy Ninje baada ya kuchelewa kuripoti kambini na baadaye kusafiri na kikosi cha Yanga kuelekea Algeria kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi USM Alger.
Kuondolewa kwa Kabwili ndani ya timu hiyo kulizua gumzo kwa baadhi ya wadau wa soka na mashabiki wakihoji ilikuwaje Kocha Ninje amuondoea ilihali ndiye kipa anayestahili kukitumia kikosi hicho.
Ikiwa ni hivo, nani atayeinusuru yanga katika mchezo wake na Prison leo. Kipa wao wakwanza kaingia mitini na huyu wapili keshajiunga na timu ya taifa cjini ya 20. Almuradi Yanga imekua kama yatima hamna baba hamna mama
ReplyDeleteYanga sasa yaporoja. Wameapa watasinda michezo yao yote oliyobaki kiopiku Simba. Wamesahau kuwa Simba katika mechi zake tatu zilibaki inatakiwa droo tu na Singida hata waveshwe taji la kifalme na kwa kila mchezaji kujaza mamilioni migukoni mwao kujitsyarisha na sherehe kubwa sana isiyotabirika
ReplyDelete