May 24, 2018


Na George Mganga

Kundi la Spora kupitia WhatsApp linaloshabikia klabu ya Simba limemkabidhi beki Shomari Kapombe zawadi ya kiasi cha shilingi laki tano (500,000) kama mchezaji bora wa mwezi Aprili 2018.

Kapombe amekabidhiwa kiasi hicho cha fedha na Kiongozi Mkuu wa kundi hilo, Ally Masaninga pamoja na fremu iliyo na picha yake katika Uwanja wa Bocco Vetarani unaotumiwa na wekundu hao wa Msimbazi kujifua kwa ajili ya mechi za ligi.

Spora wametoa zawadi ya fedha hizo kama sehemu ya kutoa motisha na hamasa kwa wachezaji wa Simba kujituma zaidi Uwanjani ili kuipigania timu iweze kupata matokeo.

Tangu msimu wa 2017/18 uanze, imekuwa ni utaratibu wa kawaida kwa kundi hilo kutoa zawadi ya mchezaji bora kwa kila mwezi inayolenga kutia morali kwa wachezaji.

Zawadi hiyo imetolewa ikiwa Simba ambao ni mabingwa wapya wa ligi msimu huu wakijiandaa kuhitimisha ratiba ya mechi za ligi Kuu Bara ambapo watacheza dhidi ya Majimaji FC Jumatatu ya wiki ijayo.





2 COMMENTS:

  1. Simba inastahiki kwa kuwa ndio timu inayowathamini wachezaji wake kuloko zote. Tumeshihudia nuora akijikwaa na kujiumiza kidole, siku yapili tu uupo India kwa matibamu na motisha ndoo usiku ns a na huko tunapoeelekea ndoo kutamu na kumenona zaidi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic