May 21, 2018




NA SALEH ALLY
WAKATI mwingine linaweza likawa ni kama jambo linaloshangaza hivi, lakini ukituliza kichwa utagundua kuna watu wanaojaribu kutaka kusahau jambo fulani ili kuziacha siku zipite.

Nimeona mitandaoni, mashabiki wengi ambao ninaamini watakuwa wanashabikia Yanga wakiwa ‘busy’ kupambana kuwazodoa Simba kutokana na kufungwa na Kagera bao 1-0.
Mashabiki hao wanaizodoa Simba kwa kuwa wamepoteza mechi moja ya Ligi Kuu Bara kwa kufungwa na Kagera Sugar, siku ambayo walikuwa wanakabidhiwa kombe.

Kama ni siku ya kukabidhiwa kombe, Simba walishakuwa mabingwa tayari. Walifanikiwa kutangaza ubingwa wakiwa na mechi tatu mkononi na tayari walishacheza moja na kubaki mbili na moja ndiyo hiyo dhidi ya Kagera Sugar iliyokuwa inapambana kujiokoa kuteremka daraja.

Mmoja wa viongozi wa Yanga, nisingependa kumtaja jina, naye alinishangaza sana kuona akipiga kelele kufurahia Simba kufungwa angalau mechi moja ya ligi kuu! Binafsi niliona ni mambo ya ajabu sana kwa mambo mawili.

Kwanza, ulikuwa ni mchezo wa kwanza Simba inapoteza wakati Yanga tayari ilishapoteza mechi nne na kuwa moja ya timu kubwa zilizopoteza mechi nyingi lakini ajabu kuona watu wanaoiunga mkono wanafurahia na kushadadia timu iliyopoteza mechi moja baada ya kuwa imetangazwa kuwa bingwa.

Pili, ajabu inaongezeka kwa kuwa siku shabiki au kiongozi wa Yanga anaonekana kufurahia Simba kupoteza mechi moja, siku hiyo pia timu yake imefungwa mechi ya tano ya ligi.

Juzi, Yanga ilikuwa imepoteza mechi ya tano ya ligi baada ya kufungwa mechi yake dhidi ya Mwadui FC mjini Shinyanga.

Wakati Simba imefungwa moja, Yanga imefungwa tano, kweli shabiki sahihi wa klabu hiyo anaweza kuinua mdomo na kuizodoa Simba? Huu ni ushabiki wa namna gani au wa aina ipi? Unashangaza kabisa!

Aliyepoteza mechi tano anaishangaa timu iliyopoteza mechi tano? Maana yake hana uchungu na klabu yake au kuna tabia mbovu ambayo tumeiendekeza ya kila mmoja kuwa ‘busy’ na vya wenzake.

Ajabu zaidi kuna uchungu mwingine, kwamba wakati Yanga imefungwa na Mwadui FC ilikuwa inapoteza mechi yake ya tatu mfululizo katika ligi kuu.

Unaona Yanga iko katika matatizo makubwa ya kifedha, kimawazo na hata ya kuungwa mkono kwa kuwa watu wao hawana habari au wanajisahaulisha kinachoendelea au wanajiondoa kwa kuwa kuna shida.

Mashabiki wanapaswa kubadilika, lazima mjue Yanga kwa shida na raha ni yenu. Msijikaushe, shughulikieni kilicho sahihi badala ya kupambana kutuliza mioyo yenu.

Yanga haifanyi vizuri, jiulizeni kwa wanachama, nyote mmelipa ada? Kwa mashabiki jiulizeni mnachangia nini kuifanya Yanga kuwa bora tena na timu ambayo itaendelea kufanya vizuri.

Yanga imekuwa timu ya kufungwa mechi tatu mfululizo? Yanga imekuwa timu isiyo na mwelekeo tena, inasafiri utafikiri timu ya ndondo kwenda kucheza michuano Tandika! Yanga imekuwa timu inacheza mechi katika benchi ina wachezaji wawili tu wa kuingia, hakuna hata kipa, mmoja ni majeruhi na mwingine ni kinda!

Kama kweli mnaipenda Yanga, ihurumieni. Achaneni na mambo ya wenzenu na mpambane kwa mioyo ya dhati kutoa misaada ambayo mnaamini itakuwa ni sahihi kwa ajili ya kuiondoa Yanga ilipo.

Lakini kwa viongozi ambao mngependa kujulikana mitandaoni, basi wakati mzuri badala ya kupiga kelele za kuona Simba imepoteza mechi moja, basi fanyeni yaliyo sahihi kuing’oa Yanga ilipokwama.

Yanga lazima isonge mbele lakini itakuwa hivyo tu kama mtabadilika na kuachana na kuwekeza nguvu kwa jirani na badala yake, zirudisheni zote kwenu.


6 COMMENTS:

  1. MHHH kumbee ehhh hya tumekuelewa

    ReplyDelete
  2. Jamaa kapiga on the spot. Hakuna longolongo wala nini.Konaball kashindwa ju comment .Mwenzetu kachukua ubingwa sisi tumebaki kupiga kelele eti kafungwa mechi moja sisi tuliotandikwa mechi tano imekuwa kawaida.Na tulivyo wajinga tunamshangilia huyo kiongozi kwa ujinga wake.Tunaweza kukosa hata nafasi ya pili kwa ujinga wetu wa kusifia ujinga.

    ReplyDelete
  3. Ndugu Saleh Jembe: Naomba sana sana nifikishie ujumbe huu kwa Boniface Mkwasa katibu mkuu wa Yanga au Clement Sanga. Yanga mnaweza kujitegemea na kuwa matajiri bila kumtegemea mtu binafsi mnapaswa tu kufanya yafuatayo: Anzisheni kampuni ya hisa ya Yanga, kampuni isajiliwe brela, kama kampuni nyingine, kampuni hii itakuwa mali ya klabu ya Yanga. Wanachama wa Yanga katika kampuni hii watamiliki hisa asilimia 51% na mwekezaji atakae jitokeza atamiliki hisa asilimia 49%. Hisa katika kampuni hii ziuzwe kwa wanachama kwa bei ya shilingi efu kumi (10,000) tu, utaratibu wa uuzaji wa hisa hizi uongozi wa Yanga uingie makubaliano ya kisheria na kampuni zote za simu kwa Tanzania bara na visiwani kuwaruhusu mashabiki na wanachama kununua hisa hizi kupitia mihamala ya simu zao za mikononi kama mpesa, tigo pesa, halopesa, airtel money, easy pesa nk pia kupitia utaratibu wa kibenki, jambo la msingi uongozi utoe akaunti maalum ya Yanga ya benki kama Crdb au Nmb ambapo mwanachama anaweza kununua au kulipa kununua hisa zake huko. Na klabu itoe namba za simu za mkononi ambapo pia mwanachama anaweza kununua hisa au kulipia. Pesa hizi za hisa ziingie kwenye akaunti ya kampuni ya hisa ya Yanga, endapo watu milioni 1 watanunua hisa kwa sh 10,000 zitapatikana shilingi bilioni 10 na endapo watu laki moja watanunua hisa hizi itapatikana bilioni moja, baada ya kupata pesa uongozi wa kampuni ya hisa ya Yanga, uanzishe shindano la bahati nasibu kama yalivyo mashindano mengine ya biko, tatu mzuka, moja bet nk, shindano hili lisajiliwe katika shirika la bahati nasibu la Taifa, washiriki wa shindano hili wanunue kila tiketi ya ushiriki kwa sh 1000 kwa tiketi 1 endapo watu laki moja watacheza kila siku zitapatikana shilingi milioni 100 kila siku ambazo ni sawa na bilioni 3 kwa mwezi pesa hizi zote zitaingia kwenye akaunti ya kampuni ya hisa ya Yanga. Washindi wa 5 watapatikana kila mwisho wa mwezi na kukabidhiwa zawadi zao jumla ya shilingi milioni 300 kila mwisho wa mwezi,ukitoa kodi na gharama za matangazo kwenye kampuni za television radio na mitandao ya simu ukitoa bilioni 1.2 utabakiwa na bilioni 1.5 pesa hii kiasi cha shilingi milioni 500 kinaweza kuwa mishahara ya wachezaji benchi la ufundi na viongozi waajiriwa wa klabu ya Yanga pamoja na kampuni ya hisa ya Yanga. Salio la sh bilioni moja (1) kila mwezi ni kwa ajili ya maendeleo na miundo mbinu ya klabu ya Yanga. Hapo nimeongelea jinsi ya kutumia zile hisa asilimia 51% za klabu ambazo ni mali ya wanachama wa Yanga, ambazo lazima wazinunue kwa mapenzi yao kwa Yanga. Kwa hisa asilimia 51% tunaona Yanga peke yake inaweza kusimama bila kuwa omba omba. Nikija kwenye hisa asilimia 49% za mwekezaji, itafutwe kampuni ambayo itaingia mkataba Yanga kutengeneza bidhaa au kutoa huduma zenye jina na nembo ya Yanga, kampuni hii ikubali kuuziwa kwa mkataba nembo ya Yanga kwa madhumuni wa kuitumia nembo hii kibiashara kwa lengo la kuitangaza kampuni hii na kuinufaisha Yanga pia. Faida igawanywe kwa makubaliano ya kimkataba kati ya kampuni hii na klabu ya Yanga. Huo ndio ushauri wangu kwa klabu ya Yanga; namna wanavyoweza kujikwamua katika hali ngumu ya kiuchumi inayowakabili hadi hivi sasa. Nawasilisha: 0756887800

    ReplyDelete
    Replies
    1. Issue ni kubadilisha katiba mkuu.kuna wazee wanajifanya kina Akilimali, Akilimbovu, Akilimingi, wanaodai hakuna mabadiliko Yanga labda wakiondoka duniani.Simba imewachukua miaka miwili kufanikisha hilo zoezi kwa mbinde.Hizo strategics unazozieleza si za leo kuzisikia.Wengi wameshaelezea na kujaribu kuelimisha lakini kuna Akilimingi wameshaapa hakuna mabadiliko.Tunabaki kushangilia timu zingine zinazoifunga Simba na wakati huo tukijua hata akipoteza mechi alizosalia bado havuliwi ubingwa wa msimu wa 2017/2018.Na zaidi ya ubingwa wamepiga hatua kubwa nyingine ya ushindi kwa kupitisha mfumo wa uendashaji wa klabu na kukimbia adha ya omba-omba.Inasikitisha

      Delete
    2. MasiQinii yaangaaa! Wanatia huruma jamaani. Si tuwaachie tu lile ndoo?? Mweeeeeh!!!

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic