MARCEL KAHEZA ATHIBITISHA RASMI KUSAINI SIMBA
Na George Mganga
Mshambuliaji aliyekuwa anichezea Majimaji FC, Marcel Kaheza, amethibisha kusaini mkataba wa awali na klabu ya Simba ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu nchini msimu huu.
Kaheza ambaye ambaye amehitimisha safari ya kuichezea Majimaji FC iliyoshuka daraja rasmi leo baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Simba, atakuwa na kikosi cha wekundu hao wa Kariakoo katika msimu ujao wa ligi.
Mshambuliaji huyo ambaye aliwahi kuichezea Simba akikuzwa kutoka kikosi B, anakuwa anarejea kwa mara ya pili Msimbazi baada ya kupachika mabao 14 kwenye ligi akiwa na Majimaji msimu huu.
Mbali na Kaheza, taarifa zimeeleza pia kuwa Simba imeshanyaka saini ya Mshambuliaji wa Lipuli FC, Sadam Salamba.
Baada ya Kaheza aliyekuwa wa kwanza kusaini na Simba, Salamba anakuwa mchezaji wa pili kujiunga na mabingwa hao mara 19 katika Ligi Kuu Vodacom.








This is simba
ReplyDeleteYanga wanaumia hata kusoma habari mpk mwisho inawatisha.
ReplyDeleteSSC INAFURAHISHA, TUNATAKA ZAIDI YA HAPO.
ReplyDeleteHawa nadhni wamewasajili kwa ajili ya Kagame na Sport pesa Cup si kwa kuwania ligi kubwa. Upumba wa aina gani viongozi wa Simba wanafanya?
ReplyDeletewewe for sure hujielewi hata alivyosajiliwaga Kichuya uliongea upumbavu huo huo...ila wewe lazima utakuwa bonge la witch(Mchawi)
Deletesaafiii sana
ReplyDeleteWachezaji hawa wazuri tu hata kwa ligi kubwa hawa ndio wachezaji wa ndani. Bado wachezaji wa nje watatafutwa wa viwango
ReplyDeleteKaka ndio wachezaji wetu mm nipo kama wewe nilikua najiuliza ili simba ifanye vizuri inaitaji wa chezaji gani?kwakweli jibu sijapata.kwamaana hata aowanao waacha kwatimu za ndai niwachezaji wa zuri
ReplyDelete