May 17, 2018


Baadhi ya mashabiki wa Yanga wameendelea kusisitiza kutohitaji huduma ya Kocha wake Msaidizi, Shadrack Nsajigwa kwa madai ya kuwa ameshindwa kuihimili vizuri.

Yanga jana imeenda suluhu ya 0-0 na Rayon Sports ya Rwanda katika mchezo wa pili wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mechi hiyo imekuwa ni ya nane kwa mabingwa hao wa zamani wa ligi kuu Tanzania Bara bila kupata ushindi kufuatia suluhu ya jana.

Ikumbukwe Yanga imetoka kufungwa idadi ya mechi tatu mfululizo katika Ligi Kuu Bara, jambo ambalo mashabiki hao baadhi wameligusia.

Wengi wameeleza kuwa ameshindwa kuisaidia Yanga kutokana na mwendelezo wa matokeo mabovu inayopata hivyo hawaoni faida ya yeye kuendelea kuwa Kocha Msaizidi.

5 COMMENTS:

  1. Pole na kazi bro Saleh.Mimi ni miongoni WA wafuatiliaji wazuri sana WA blog yako kwa ajiliajili ya kupashwa habari mbalimbali za michezo..Msema kweli mpenzi wa Mungu,bro siku hizi habari zako ziko too shallow..Kwa mfano hii ya leo Mr.Nsajigwa akisoma atadhani ni maoni yako binafsi sababu hujaweka maneno ya hao mashabiki wasiomtaka nsajigwa(quatation)..Jitahidi kuongeza ujazo kwenye habari zako...tuko pamoja..Ramadhan Mubarak kaka mkubwa.

    ReplyDelete
  2. YA NSAJIGWA SAWA NA KESSY PIA ANATUGHARIMU KWA KUTOKUWA NA NIDHAMU MCHEZONI. NI BORA AKAPEWA UNAHODHA TUJUE MOJA MAANA KADI ANAZOPATA KWENYE MECHI NI KWA SABABU ANAONGEA NA REFA KULIKO NAHODHA. MWASHIUYA ALISHINDWA KABISA ZAIDI YA KUONYESHA HASIRA KWA REFA. KULIKUWA NA FAIDA GANI KUMWINGIZA MARTIN DAKIKA MBILI KABLA YA MCHEZO KWISHA.

    ReplyDelete
  3. Kocha anafanya kazi bila mshahara. Toeni pesa kununua kocha mnayemtaka. Msisahau tatizo lenu la msingi kwa kushughulika na dalili tu🐸🐸🐸

    ReplyDelete
  4. YANGA.....YANGA...YANGA...::
    Hii ni aina ya ukataji wa tamaa ambao unaendelea kuonesha kutokana na uwajibikaji mbovu wa baadhi ya watu ndani ya Timu. Timu imekosa morali..timu imekosa muelekeo...timu inatia huruma...Masikitiko sana.

    Unaingalia Yanga SC na kundi lililopo...unajisemea mwenyewe.."""tungepata hili kundi miaka miwili iliyopita..tungetoboa"""....hii ni kauli ya mashabiki. Yanga imekosa mvuto..Yanga imekosa muelekeo..Yanga inafuata upepo sasa....imepotea.

    Kipindi cha mapumziko wachezaji wanachelewa kurudi uwanjani...hatuoni dalili za watu...unajiuliza.."""kuna nini ndani ya vyumba vya kupumzikia...nini kilikuwa kinaendelea??"""...hii si Yanga SC tunayoijua...Yanga sumbufu....Yanga inaamua matokeo...Yanga ya Mbuyi Twite...Yangaaaa.

    Kocha anamuanzisha Mhadhi....na Mwashiuya...anamuweka nje Daud na Martin....watu waliokosa mvuto ndani ya mashabiki wengi wa Yanga. Kocha anafanya mabadiliko dakika tano hadi kumi za mwisho...Yanga SC imekosa maamuzi sasa...hili ndio tatizo la kumtegemea mtu...Yangaaaa!!!!Yanga majanga.

    Yanga SC imepewa fursa ya kutafuta wachezaji watatu wa kuwaazima na si kununua...kikubwa ni kuongea na uongozi wa vilabu vyao na kuwatumia...Yanga mmeshindwa hata kwenda Singida United????viongozi mmeshindwa hata kumuomba Mwigulu Njemba aongee na viongozi wake wa Singida kuwaadhima wachezaji....???hii Yanga gani hii???

    Yanga SC ya tangu mechi ya Township Rollers ile ya Gaborone wanatumia striker mmoja...Chirwa tu ndio anasubuka pale mbele...Yanga imekosa matured players...hasa kipisi cha mbele...watu hawapambani hataaaa...hataaaa...hataaa!!!hii hatari.

    Mmetufanya washabiki na wanachama wenu wapumbavu..yaani mnatupumbaza kwa maneno ya vifaranga vya kuku na mamaye ""mtanyonya kesho""...Yanga SC viongozi si wabunifu hata chembe. Moja ya sehemu inayofanya vibaya ni kipande cha Ushmbuliaji...!!

    USHAURI WANGU::
    Nifikishie hili suala kwa uongozi wa Juu wa Yanga ukiongozwa na Mjomba angu Mkwasa. Naomba wafanye haya.;;;--

    Tukae na Singida United...tupeleke barua....tuwaombe wachezaji watatu wa mbele...yaani Pappy Kambale, Lubinda Mumbia na Kotinyo...hawa watu watatu kwanza wanajuana...watacheza pale mbele wakati Chirwa ataenda pembeni kama winga. Kwahiyo timu itakuwa kama ifuatavyo:::-
    1) Rostand
    2) Kessy
    3) Gadiel
    4) Dante
    5) Kelvin
    6) Kamusoko/Tshishimbi
    7) Chirwa
    8) Kotinyo
    9) Kambale
    10) Lubinda Mumbia (Mbia)
    11) Buswita/Martin

    Naamini kwa uwiano wa wachezaji mechi ya Ryon ya marudio tunaweza kufanya kitu na hata Gor Mahia. Jana Yanga ingeshindwa ingepata point tatu na kwenda kataika nafasi ya pili. Hawajachelewa kutokana na aina ya Viwango sasa ni kupambana kupata watu hao watatu..tuachane na fikra za Salamba atakuja atashindwa nae kupafom kutokana na ubutu wa uwiano wa wachezaji.

    Yangu ni Hayo::
    Alex Mwamjengwa

    ReplyDelete
  5. Mnamvisha Koti lisilolake Msajigwa.Mwenye koyi la kulaumiwa Zysnga di msajigwa.Kwanza wachezaji wanaidai yanga.Je msajigwa ndie awalipr wachezsji? Kwa kutolopwa kunafanya wavhezajk wsvheze kwa kiwango duni.Uongozi wa Yanga chini ya mkwasa nfio wenyekoyk la angukk la Yanga.mkichelewa kung'oa hao yanga inaelekea pabsya.Msajigwa afsnyeje.semeni kweli.hata ajd generali wa man vity ,( gadiola,). Au huyo kocha wanayetamba naye simba.apewe kikksi chenye madai ya muda mrdfu klsbuni.timu haiwezi kusogea. Hivyo ni akina Mkwasa ndio wsnaochezea akilk za wnayanga.hao ni wapigsji tu...wana ysnga wawajue wanao waangusha.msiwazunguke wahudika wa anguko ls yanga kwa kumvisha Msajigwa Zkkti ljsilo lake

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic