May 16, 2018



Na George Mganga

Bodi ya Ligi kupitia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imeufanyia mabadiliko mchezo namba 226 wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba SC dhidi ya Kagera Sugar.

Mchezo huo awali ulipaswa kuchezwa Jumapili ya Mei 20 2018 lakini sasa umefanyiwa mabadiliko na utapigwa Jumamosi ya Mei 19 2018.



Mechi hiyo inatarajiwa kuanza majira ya saa 8 kamili za mchana ukienda sambamba na hafla ya kuikabidhi Simba kombe la ligi ililolitwaa msimu huu wa 2017/18 ikiwa imejikusanyia alama 68.

Sababu za mabadiliko ya ratiba hiyo ni kuongezwa kwa ufanisi wa kulibadhi taji hilo la ligi kwa Simba huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akitarajiwa kuwa mgeni rasmi.


1 COMMENTS:

  1. Simba bana mambo yao makubwa makubwa mnanifuragishaga yani nyie tu hamjui sasa tunataka kombe mabingwa wa Africa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic