Na George Mganga
Katika mchezo huo uliopigwa Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam, Mali walikuwa wa kwanza kufunga bao mnamo dakika ya 33 kupitia kwa Ousmane Diakite na baadaye katika dakika ya 41, Samadiare Dianka akaongeza la pili.
Bao pekee la kusawazisha kwa Ngorongoro limetiwa kimiani na Paul Peter kwenye dakika ya 42.
Katika mchezo huo, Kocha Mkuu wa Ngorongoro, Ammy Ninje alimuweka benchi kipa Ramadhani Kabwili na kumpa nafasi Mzanzibari kutoka JKU, Peter Mashauri kucheza nafasi hiyo.
Kutokana na matokeo hayo, Ngorongoro italazimika kushinda mabao mawili kwa sifuri katika mchezo wa marudiano utakaopigwa mjini Bamako, Mali, Mei 20 2018.
Ninje anamuwekaje benchi KABWILI wakati anajua kabisa dogo ndiye anauzoefu kimataifa na hiyo milingoti mitatu?
ReplyDeletekabwili mimi binafsi niliiona nafasi yake.
ReplyDeleteninje kaweka bifu ambalo linakosesha ushindi. magoli simpo sana wamefunga mali
DeleteWe acha tu watanzania yamebakia yetu macho tu na jinsi mambo yanavyokwenda kwenye timu zetu za taifa. Kama kusema watu walishasema sana lakini wahusika kana kwamba hawajali.
ReplyDelete