May 14, 2018



Na George Mganga

Kikosi cha Rayon Sports kimewasili nchini kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa Mei 16 dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Rayon wamewasili nchini baada ya kwenda sare ya 1-1 dhidi ya Gor Mahia FC katika mchezo wake wa kwanza uliopita wa hatua ya makundi uliopigwa Amahoro Stadium jijini Kigali Rwanda.

Kuelekea mchezo huo tayari viingilio vimeshatajwa ambapo VIP A itakuwa Tshs 15,000, VIP B na C ni 7000 na mzunguko itakuwa ni Tshs 3000 pekee.

Yanga itakuwa inapambana kupata matokeo mazuri ili kujitengeneza mazingira ya kuendelea kusalia kwenye michuano ya kimataifa endapo itafanikiwa kubwa bingwa.

Ikumbukwe Yanga ilipoteza mchezo wake kwa kwanza kwa jumla ya mabao 4-0 dhidi ya USM Alger uliopigwa jijini Algiers huko Algeria.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic